George Binagi-GB Pazzo @BMG.
Wakazi
wa Jiji la Mwanza wameingia katika taharuki baada ya kutokea uvumi wa
taarifa za mti kugoma kung’olewa katika eneo la Pasiansi ambapo kuna
shughuli ya upanuzi wa barabara inayoelekea uwanja wa ndege wa Mwanza.
Taharuki
hiyo ilianza tangu jana majira ya jioni ambapo mamia ya wananchi
walijazana katika eneo hilo ili kushuhudia mgomo wa mti huo ambao
inasadikika ulikuwa ukitoa sauti za kulalama mithiri ya binadamu.
Zoezi
la kuung’oa mti huo aina ya mwembe limefanikiwa hii leo majira ya saa
tatu asubuhi baada ya shughuli pevu ya kuung’oa kwa kutumia mashine aina
ya burudoza huku baadhi wakihusisha tukio hilo na imani za kishirikina
na wengine wakisema ni upotoshaji tu ulifanyika juu ya tukio hilo.
Kasim
Mlisu ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya ujenzi ya Nyanza Road Works
inayojenga barabara ya Pasiansi, amesema taarifa za mti huo kuzungumza
ni za upotoshaji na kwamba zoezi la kuung’oa lilichukua muda mrefu tangu
juzi ili kupisha hatua za upimaji wa ukubwa wake na kusubiri mashine
aina ya“skaveta” iliyofanikiwa kuung’oa.
Katibu
wa Chama cha Tiba asilia mkoani Mwanza CHAWATIATA, Kawawa Athuman,
amesema tukio la mti kuzungumza ama kugoma kung’olewa halina ukweli
wowote kwa karne hii ya 21 japo matukio ya aina hiyo yalikuwepo enzi za
kale kabla ya ujio wa dini barani Afrika ambapo amewatahadharisha
watumiaji wa mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kujiepusha na
usambazaji wa taarifa za upotoshaji.
Zoezi la kuung'oa mti likiendelea
Hapa msumeno ulikata ila mti ukagoma kuanguka licha ya kuvutwa
Zoezi la kuung'oa mti huo likiwa limefanikiwa
Zoezi la kuung'oa mti huo likiwa limefanikiwa
Zoezi la kuung'oa mti huo likiwa limezaa matunda
Katibu wa Chama cha Tiba asilia mkoani Mwanza CHAWATIATA, Kawawa Athuman, akizungumzia tukio hilo
Kasim Mlisu ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya ujenzi ya Nyanza Road Works akizungumzia tukio hilo
Wakazi wa jiji la Mwanza wakifuatilia tukio hilo
Wakazi wa jiji la Mwanza wakichukua tukio hilo
Wanahabari na wakazi wa jiji la Mwanza wakichukua tukio hilo
Wanahabari na wakazi wa jiji la Mwanza wakichukua tukio hilo
Kushoto ni dereva aliyekuwa akiendesha mtambo uliong'oa mti huo
SHARE
No comments:
Post a Comment