Maandamano makubwa
yanashuhudiwa kote nchini Mexico, baada ya mauaji ya mwandishi maarufu
wa habari za upekuzi, na mshindi wa tuzo mbalimbali, Havier Valdez,
ambaye alitumia miaka mingi kufichua taarifa za magenge ya walanguzi wa
dawa za kulevya.
Vyombo vya habari na watetezi wa haki za binadamu nchini humo wameungana na kuwa kitu kimoja kinachopinga tukio hilo.
Valderz aliandika kwa upana kuhusu watumiaji wa madawa, na Rais Enrique Pena Nieto ametaja kifo chake kama kosa la kikatili.
Mara kwa mara walichapisha sura ya Valdez ambae aliuawa karibu na ofisi za gazeti na alipatikana nyumbani kwake Culiacan katika jiji la Sinaloa.
Mexico inatajwa kama nchi ya tatu hatari zaidi kwa usalama wa waandishi wa habari duniani, huku waandishi watano wakiwa wameuawa mwaka huu.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment