Mjumbe wa Bodi wa Mfuko wa Fidia
kwa Wafanyakazi (WCF) Dkt. Francis Michael akifungua Semina ya
uelimishaji kwa Waajiri kuhusu haki na wajibu wa mwajiri na mfanyakazi
jijini Morogoro leo (jana), kulia ni Mwanasheria Mwandamizi Bi. Irine
Mungu.
Mwanasheria Mwandamizi Bi. Irine
Mungu kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) akitoa mada kwa
waajiri kuhusu haki na wajibu wa mwajiri na mfanyakazi jijini Morogoro
leo (jana)
Afisa Uhusuano Mwandamizi kutoka
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) akitoa mada katika semina ya
uelimishaji kwa waajiri kuhusu haki na wajibu wa mwajiri na mfanyakazi
mkoani morogoro leo (jana)
Bw. Fabian Felician akichangia
mada katika semina ya uelimishaji kwa waajiri kuhusu haki na wajibu wa
mwajiri na mfanyakazi iliofanika mkoani Morogoro leo (jana).
Afisa Kazi Mfawidhi mkoa wa
Morogoro Bw. Simbo Swai akichangia mada katika semina ya uelimishaji kwa
waajiri kuhusu haki na wajibu wa mwajiri na mfanyakazi iliyofanyika
mkoani Morogoro leo (jana).
Bi. Hilda Msemo kutoka Mzinga
Corporation akichangia mada katika semina ya uelimishaji kwa waajiri
kuhusu haki na wajibu wa mwajiri na mfanyakazi iliyofanika mkoani
Morogoro leo (jana).
Baadhi ya washiriki wa semina ya
uelimishaji kwa waajiri wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi wa
semina hiyo ambaye ni Mjumbe wa Bodi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi
(WCF) Dkt. Francis Michael mkoani morogoro leo (jana).
…………………..
Na Idara ya Uhusiano na Mawasiliano (WCF).
Morogoro.
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi
(WCF), umeendesha semina ya siku moja kwa waajiri nchini katika mikoa
minne, ili kutoa elimu juu ya shughuli za Mfuko na wajibu wa waajiri kwa
wafanyakazi wao katika kujisajili na kuwalipa michango kwa niaba ya
waajiriwa wao.
Akizungumza katika semina hiyo mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko Dkt. Francis Michael .
Amesema kuanzishwa kwa mfuko huo
kumekuja wakati muafaka ambapo Tanzania inaelekea katika uchumi wa
viwanda hivyo kupelekea ongezeko la wafanyakazi ambapo chombo hicho ndio
mkombozi wa majanga yatokanayo na kazi.
“Ni muda muafaka kwa waajiri
kutambua wajibu wenu katika Mfuko huu na pia kutambua madhara ya
kutotekeleza wajibu wenu” Alisema Dkt. Michael.
Katika hotuba yake, Dkt.
Michael alieleza umuhimu wa waajiri kuwalipia michango wafanyakazi wake
kama sheria inavyotaka, ili kuwawekea akiba pindi wapatapo na majanga
wakiwa kazini.
Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi
ni Taasisi ya Serikali chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na umeundwa kwa
mujibu wa kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi Sura ya 263
iliyorejewa Desemba, Mwaka 2015.
Dkt. Michael amesema, Mfuko
umeamua kuandaa semina hiyo ili kutoa elimu zaidi kwa waajiri kwa
kutambua kuwa waajiri ndio wadau wakuu wa Mfuko huo na semina hiyo
itawasaidia kujua kazi za Mfuko lakini pia wajibu wa waajiri kwa
wafanyakazi katika kutoa michango ya kila mwezi.
Akitoa mada juu ya Mfuko wa
Fidia kwa Wafanyakazi, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Sebera
Fulgence, alisema, Mfuko huo upo kisheria ili kutoa fidia kwa
wafanyakazi watakaoumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi.
Naye Mwanasheria Mwandamizi wa
Mfuko huo Bi.Irene Mungure amesema, ni muda mwafaka kwa waajiri
kutambua wajibu wao katika mfuko ikiwa ni pamoja na kutambua madhara ya
kutokutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa Sheria.
Katika uzinduzi wa semina
hizo jana Makao Makuu ya Nchi Dodoma, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw. Emmanuel Humba, alifafanua
zaidi juu ya haja ya waajiri kuufahamu vizuri Mfuko namna unavyoendeshwa
ikiwa ni pamoja na kulipa fidia kwa wafanyakazi watakaoumia, kuugua ama
kufariki. Aidha, alisema kuwa waajiri ni wadau wakuu wa uendelezaji
Mfuko.
Bw. Humba aliwaasa waajiri
kutokufanya udanganyifu na ubadhilifu hasa katika uwasilishwaji wa
michango kwani itakuwa ni kuudidimiza Mfuko na ni kosa kisheria na
waajiri watakaojihusisha watachukuliwa hatua za kisheria kwa mujibu wa
Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi Sura ya 263 iliyorejewa Desemba, Mwaka
2015
Semina hiyo imefanyika katika mikoa ya Dodoma,Kilimanjaro, Morogoro na Arusha.
SHARE
No comments:
Post a Comment