TRA

TRA

Tuesday, May 9, 2017

Mgombea urais Korea Kusini aahidi kuimarisha uhusiano na Korea Kaskazini

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !




http://www.straitstimes.com/sites/default/files/articles/2017/03/13/41874245.1_41874931_-_12_03_2017_-_skorea-politics.jpg
SEOUL, Korea Kusini
KATIKA hali ambayo si ya kawaida, mgombea wa nafasi ya urais nchini kupitia chama cha Liberal, Moon Jae-In ameahidi kwamba endapo atafanikiwa kuibuka mshindi ataimarisha uhusiano na Korea Kaskazini.

Kauli hiyo ya Jae-In (pichani) inakuja wakati mamilioni ya wananchi nchini, leo walijitokeza kupiga kura kuchagua rais ambaye anatarajiwa kuchukua nafasi ya Park Geun-Hye ambaye aliondolewa madarakani baada ya kufunguliwa mashtaka ya ulaghai akiwa madarakani.
Uchaguzi huu unakuja katika kipindi ambacho kumekuwako na mdororo wa uchumi na uhusiano mbaya na nchi jirani ya Korea Kaskazini ambayo imekuwa ikitishia kulishambulia taifa hili kwa makombora yake.
Jae-In katika kampeni zake, amekuwa akiinadi sera hiyo ya kuimarisha uhusiano na taifa hilo na kusababisha baadhi ya vyombo vya habari Korea Kaskazini, kueleza kwamba wakazi wa taifa hilo wangependelea kuona uongozi mpya wa taifa hili ukirejelea maisha ya zamani ambapo mataifa haya mawili yalikuwa ya kishirikiana na kuwasiliana.
Mgombea huyo anayeegemea mrengo wa kushoto yuko kifua mbele, huku yule mwenye msimamo wa kadri Ahn Cheol-soo akiwa mpinzani wake mkubwa.
Moon anataka kuimarisha mawasiliano na Korea Kaskazini kinyume na aliyekuwa kiongozi wa taifa hili, Geun Hye ambaye alikata uhusiano wote na taifa hilo.
Wachambuzi wa mambo wanatarajia idadi kubwa ya watu kujitokeza huku idadi hiyo ikipigwa jeki na wapiga kura vijana huku Korea Kusini ikichagua rais kutoka kwa wagombea 13.
BBC

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger