MJUMBE Maalum wa mzozo wa Libya, Rais
Mstaafu wa awamau ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na
Waziri Mkuu na Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Libya Mhe. Fayaz
Serraj jijini Tripoli, nchini Libya Mei 10, 2017. Dkt.Kikwete anaendelea
na usuluhishi wa kutafuta suluhu ya mzozo wa ,iutawala nchini humo
ambapo pamekuwa na makundi kadhaa yanayopigana tangu kuuawa kwa rais wa
nchi hiyo Kanali Muaamar Gadaf. Mjumbe huyo wa AU, alitarajiwa kufanya
mazungumzo na wadau mbalimbali katika mzozo huo.
Akiwa jijini Tripoli, Rais Mstaafu na ujumbe wake kutoka Kamisheni ya Umoja wa Afrika amekutana na Waziri Mkuu na Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Libya Mhe. Fayez Serraj na Rais wa Baraza Kuu la Libya (High State Council) Mhe Abdulrahman Asswehly.

SHARE
No comments:
Post a Comment