Mkutano wa 34 wa Dharura wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam umefikia tamati. Mkutano huu uliofanyika katika Hoteli ya Serena umehudhuriwa na Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka nchi wanachama, watendaji mbalimbali kutoka Wizara, mashirika ya umma, Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, na taasisi mbalimbali za Serikali ndani ya Jumuiya.
Pamoja
na mambo mengine Mkutano huu ulikuwa ni maalum kwa ajili ya kuandaa
agenda zinazo hitaji maamuzi ya Wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki. Agenda hizo zinatokana na taarifa ya utekelezaji wa maagizo
na maelekezo mbalimbali ya Mkutano uliopita wa Wakuu wa nchi wa Jumuiya
wa mwaka 2015/2016, iliyo andaliwa na Mkutano wa ngazi ya wataalamu.
Baadhi
ya mambo yaliyopo kwenye taarifa hiyo ya utekelezaji wa maagizo na
maelekezo mbalimbali ya Mkutano uliopita wa Wakuu wa nchi wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki ya mwaka 2015/2016 ambayo imekabidhiwa kwa Baraza la
Mawaziri yanajumuisha mambo yafuatayo;
·
Taarifa ya namna ya kuwezesha uundaji wa magari katika Jumuiya ya
Afrika Mashariki na kupunguza uagizaji wa magari yaliyotumika kutoka nje
ya Jumuiya
· Taarifa ya mapitio kuhusu sekta ya nguo na ngozi juu ya kuzuia/kuondoa uagizaji wa nguo na viatu vilivyotumika na;
· Taarifa ya namna endelevu ya Uchangiaji wa bajeti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Aidha
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi
Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na wanahabari punde baada ya mkutano
amesema Mkutano huo wa Baraza la Mawaziri umekuwa na mafanikio makubwa
kwanza, kutokana na idadi kubwa na yakuridhisha ya wajumbe walioshiriki
Mkutano kutoka nchi wanachama ,na pili ni kutokana na mafanikio makubwa
yaliyopatika katika kipindi chote cha miaka miwili ambayo Tanzania
ilikuwa mwenyekiti wa Jumuiya hadi sasa inapokabidhi kwa nchi ya Jamhuri
ya Uganda.
Mfanikio yaliyopatikana katika kipindi cha uwenyekiti;
Waziri
Mahiga ameyataja mafanikio yaliyopatikana ndani ya kipindi cha miaka
miwili Tanzania ikiwa mwenyekiti wa Jumuiya kuwa ni; kuongezeka kwa nchi
ya Sudan Kusini katika Jumuiya, kuboreka kwa mfumo wa elimu kwa ngazi
ya elimu ya juu katika Jumuiya na kupungua kwa vikwazo vya biashara
vinavyotokana na vikwazo visivyokuwa vya kiforodha ndani ya Jumuiya
vilivyopelekea kurahisisha na kuhamasisha baishara katika Jumuiya.
Mkutano
huu wa Baraza la Mawaziri utafuatiwa na Mkutano wa 18 wa Kaiwada wa
Wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uanaotarajiwa kufanyika
tarehe 20 Mei, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Pamoja
na mambo mengine Mkutano wa Wakuu wa nchi unatarajiwa kupokea ripoti ya
usuluhishi ya kamati inayoongozwa na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamini William Mkapa.
Tanzania
ilikabidhiwa uwenyekiti wa Jumuiya mwishoni mwa mwaka 2014 katika
Mkutano wa Wakuu wa Nchi uliofanyika Nairobi, Kenya; na ikapewa tena
nafasi ya kuendelea kushikilia kiti hicho mwaka 2015, ambapo mpaka sasa
Tanzania wakati inaelekea kukabidhi nafasi hii ya uwenyekiti kwa nchi ya
Uganda, Tanzania imekuwa mwenyekiti wa Jumuiya kwa kipindi cha miaka
miwili mfululizo.
Waheshimiwa
Mawaziri wa Tanzania waliohudhuria Mkutano wakiwa wamesimama wakati
wimbo wa Afrika Mashariki unapigwa kabla ya kuanza kwa Mkutano
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt.
Augustine Mahiga akizungumza wakati wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri la
Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Hotel ya Serena jijini Dar es
Salaam
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt.
Augustine Mahiga akisalimiana na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wamasuala
ya Afrika Mashariki wa Uganda Mhe.Dkt.A.M Kirunda Kivejinja kabla ya
kuanza kwa Mkutano wa Baraza la Mawaziri uliofanyika Hoteli ya Serena
Jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi
Dkt. Aziz P. Mlima (wakwanza kushoto) akifuatilia Mkutano.
Balozi
wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Pindi Chana (wakwanza kushoto)
akifuatilia Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika
Mashariki
SHARE
No comments:
Post a Comment