Rais
Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete akifanya mazungumzo na Mwakilishi wa Umoja
wa Mataifa katika Mgogoro wa Libya Balozi Martin Kobler jijini Algiers
Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete akitoa msimamo wa Umoja wa Afrika kuhusu Mgogoro wa Libya .

Rais Mstaafu katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Congo na Mwenyekiti wa AU Mhe. Jean-Claude Gakosso. Kushoto ni Mkuu wa Ofisi ya Uwakilishi wa AU kwa Libya Bi. Wahida Ayari .

Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete akitoa msimamo wa Umoja wa Afrika kuhusu Mgogoro wa Libya .

Rais Mstaafu katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Congo na Mwenyekiti wa AU Mhe. Jean-Claude Gakosso. Kushoto ni Mkuu wa Ofisi ya Uwakilishi wa AU kwa Libya Bi. Wahida Ayari .
Rais
Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa
Afrika katika Mgogoro wa Libya ameendelea na juhudi zake za usuluhishi
wa mgogoro wa Libya kwa kushiriki katika Kikao cha 11 cha Mawaziri wa
Nchi Jirani na Libya kilichofanyika jijini Algiers, Algeria tarehe 8
Mei, 2017.
Katika Kikao
hicho, Rais Mstaafu amepongeza juhudi zinazoendelea za kupatanisha pande
zinazogombana nchini Libya na mafanikio yanayopatikana ikiwemo
kuimarika kwa hali ya usalama, kudhibitiwa kwa vitendo vya kigaidi,
kuongezeka kwa shughuli za uzalishaji wa mafuta na kufufuliwa kwa
mawasiliano kati ya pande zinazohasimiana.
Ameunga
mkono jitihada zinazochukuliwa na nchi za Algeria, Misri, Tunisia na
UAE katika kuhimiza mazungumzo ya Amani. Amesisitiza umuhimu wa pande
mbili za mgogoro kuheshimu Makubaliano ya Amani ya Libya (Libya
Political Agreement) na kutekeleza vipengele vyake bila ajizi.
Akiwa
jijini Algiers, Rais Mstaafu amefanya pia mazungumzo na Waziri wa Mambo
ya Nje wa Congo anayemuwakilisha Mwenyekiti wa Kamati wa Wakuu wa Nchi
za Umoja wa Afrika kuhusu Libya Mhe Jean-Claude Gakosso na
Balozi Martin Kobler, Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa na Mkuu wa Ofisi
ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia Mgogoro wa Libya (UNSMIL).
Rais Mstaafu anatarajiwa kumalizia ziara yake nchini Libya kukutana na viongozi wakuu wa pande zinazotofautiana nchini humo.
SHARE










No comments:
Post a Comment