TRA

TRA

Tuesday, May 9, 2017

Mshindi wa Milioni 10 atangaza kuuaga umasikini

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Meneja Masoko wa BIko Goodhope Heaven mwenye fulana ya njano akionyesha nyaraka zilizowekwa kiasi cha Sh Milioni 10 kwa ajili ya mshindi wao wa wiki, Emmanuel Philipo aliyeibuka na ushindi wa mamilioni hayo kutoka kwenye bahati nasibu ya Biko. Kushoto kwa Heaven ni Philipo akifuatiwa na Afisa wa NMB na kulia ni Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage.

Mshindi wa MIlioni 10 Biko aahidi kuuaga umasikini

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MSHINDI wa Sh Milioni 10 wa droo ya nne ya mchezo wa kubahatisha wa BIko
IJue Nguvu ya BUku, Emmanuel Philipo, ametangaza rasmi nia yake ya kuuaga umsikini baada ya kukabidhiwa fedha zake jumla ya Sh Milioni 10.

Makabidhiano hayo yalifanyika jana jijini Dar es Salaam kwa kuhudhuriwa na baadhi ya wataalam wa benki ya NMB kwa ajili ya kumuelimisha mashindi huyo wa bahati nasibu ya Biko ili azitumie vizuri fedha zake.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Philipo alisema kwamba ni wakatiwake
wa kuuaga umasikini kwa sababu amepata nafasi ya kutimiza ndoto zake kiuchumi kwa kuhakikisha kwamba anakamilisha mradi wake wa garage ya kutengenezea magari katika viunga vya jiji la Dar es Salaam.
Meneja Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage akionyesha namba za kucheza bahati nasibu yao inayofanikisha ushindi wa mamilioni kutoka kwa Watanzania, ambapo droo iliyopita alitangazwa Emmanuel Philipo ambaye jana alipewa kiasi cha Sh Milioni 10.
Mazungumzo yakiendelea baada ya makabidhiano hayo.
Afisa wa NMB akizungumza jambo na mshindi wa Sh Milioni wa Biko, Emmanuel Philipo baada ya kukabidhiwa Sh Milioni 10 zake kutoka Biko.
Afisa wa NMB akimkabidhi nyaraka mshindi wa Sh Milioni 10, Emmanuel Philipo katikati akishuhudiwa na Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven.
Alisema fedha alizopata jumla ya Sh Milioni 10 ni nyingi, huku akizipata kwa sababu ya kushiriki bahati nasibu ya Biko, akiamini kuwa ni mpango wa Mungu kumpatia fedha hizo ukizingatia kuwa ni wengi wanaocheza bahati nasibu.

"Namshukuru Mungu kwa kuniletea zawadi hii kwa kuwatumia wachezeshaji wa biko, hivyo ni wakati wangu wa kufanikiwa kimaisha kwa sababu ndio dhamira yangu kuu kupiga hatua kubwa kimaendeleo kwa kuamua kucheza bahati nasibu hii kwa njia yaujumbe wa maandishi kwa kufanya muamala kwenye simu za Tigo, Vodacom na Airtel ambapo namba ya kampuni niliweka 505050 na ile ya kumbukumbu niliingiza 2456 na kutangazwa mshindi mwishoni mwa wiki.

"Nawaomba Watanzania wenzangu tuendelee kuthubutu katika fursa mbalimbali
ikiwamo ya kucheza mchezo wa Biko kwa sababu sio tu zawadi zao mbalimbali
kama vile Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000 na Sh MIlioni Moja za papo
kwa hapo zinaeleweka, bali pia hata unapotangazwa mshindi wa Sh Milioni 10,
huwa wanakabidhi haraka kwa mshindi wao," Alisema.

Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven alimpongeza Philipo kwa
ushindi huo na kumtaka awe balozi mzuri kwa Watanzania wote kwa ajili
ya kuwapa elimu ya kuhakikisha kuwa wanacheza Biko ili nao waibuke na
mamilioni ya Biko.

Naye Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage, alisema
ushindi kwenye bahati nasibu yao ni mwepesi na kila mchezaji anaweza
kuibuka na fedha kutoka kwenye bahati nasibu yao ya Biko.

"Huu ni muda wa kulala masikini na kumka tajiri, hivyo njia ya ushindi ni
kucheza mara nyingi zaidi ambapo kila tiketi moja inayopatikana kwa sh
1000 inatoa nafasi mbili za ushindi wa papo kwa hapo pamoja na kuingia
kwenye droo kubwa ya wiki ya kushinda Sh Milioni 10," Alisema.

Philipo ni mshindi wa nne wa Sh Milioni 10 ambapo jana alikabidhiwa fedha
zake kwa ajili ya kuanza matumizi kama walivyokabidhiwa wenzake kutoka

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger