TRA

TRA

Thursday, May 18, 2017

MWALIMU COMMERCIAL BANK PLC (MCB), YAZINDUA KAMPENI YA WEKA AKIBA NA USHINDE, WATEJA KUONDOKA NA IPADS

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank PLC, Bw. Ronald Manongi, (katikati), akiwa na Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko, Bw. Valence Luteganya, (kulia) na Meneja Masoko, Bi. Rahma Ngassa, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mei 18, 2017.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MWALIMU Commercial Bank PLC imezindua kampeni  ya “Weka Akiba na Ushinde” kwa Wateja wake na wananchi kwa ujumla.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mei 18, 2017 wakati akizindua kampeni hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank PLC, Bw. Ronald Manongi alisema, “Draw hiyo ipo wazi kwa wateja wote waliopo na watakaojiunga na sifa kubwa ya kuingia kwenye draw hiyo ni kwa mteja aliyepo au anayejiunga, kuweka akiba ya Shilingi 50, 000 au zaidi.” Alisema Bw. Manongi.
Akifafanua zaidi Afisa huyo Mtendaji Mkuu wa benki hiyo alisema, kampeni hiyo ambayo itawawezesha wateja kupata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali kila mwezi kwa kipindi cha miezi miwili.
“Mteja anapoweka akiba (fedha), kiasi cha Shilingi 50,000 au zaidi, atapata alama, (Point) moja itakayomuwezesha kushiriki kwenye draw.” Alisema.
Alisema, kadiri Mteja anapoweka akiba zaidi ndivyo Anavyojiwekea nafasi nzuri ya kushinda zawadi mbalimbali ikiwemo IPADS na vocha za manunuzi zenye thamani ya Shilingi 100,000 na kwamba kila itakapochezeshwa droo hiyo, washindi wataondoka na zawadi mbalimbali.
Akielezea hudma za benki hiyo, Bw.Manongi alifafanua kuwa  Mwalimu Commercial Bank inatoa gharama nafuu na rafiki za kibenki na ni suluhisho la kifedha kwa walimu, watumishi wa serikali na wananchi kwa ujumla na kutoa wito kwa Wateja wapya kuja kufungua Akaunti na kuweka akiba ili wapate nafasi ya kuingia kwenye droo hiyo.
Naye Mkuu wa kitengo cha Biashara na Masoko wa Benki hiyo, Bw. Valence Luteganya alisema, “Huduma za kibenki za MCB ni bora na  nafuu, tunawahakikishia wateja wetu waje kufanya maamuzi ya kifedha yaliyo sahihi kwani tunatoa huduma mbalimbali za kibenki zilizo nafuu.” Alisema na kuongeza kuwa MCB pia inatoa huduma za ATM zilizounganishwa na mtandao wa Umoja switch ambao una ATM zaidi ya 200 nchi nzima.
“Lakini si hivyo tu pia huduma bora za kibenki kupitia simu za mkononi (Mobile Banking), huduma ya bure ya ujumbe wa SMS ukiwa na usalama na kuwawezesha wateja kupata taarifa za mara kwa mara kuhusiana na Akaunti zao. Hivyo natoa wito kwa wananchi kwa ujumla kuja na kujiunga na Benki yetu kwa huduma bora na za uhakika.” Alisema.   

 Bw. Manongi akizungumzia kampeni hiyo
 Mkuu wa kitengo cha Biashara na Masoko wa Benki hiyo, Bw. Valence Luteganya, akifafanua jinsi kampeni hiyo itakavyofanyika
 Meneja Masoko wa benki hiyo, Bi. Rahma Ngassa,(kushoto), akizungumzia ubora wa huduma za kibenki kwenye benki hiyo. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa MCB, Bw. Manongi
 Mkutano ukiendelea
 Waandishi wa habari wakiwa kazini
 Bw. Manongi akisikiliza maswali ya waandishi
 Bw. Manongi, (kushoto), akiwa na Bw.Luteganya

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger