Ndege mbili za kijeshi za China zimeizuia 'vibaya' ndege ya Marekani kulingana na jeshi la Marekani.
Ndege
hiyo inayohusika na kufanya uchunguzi, ilikuwa katika safari yake ya
kutaka kugundua mionzi katika anga ya kimataifa iliopo mashariki mwa
bahari ya China.Ndege hiyo ilikuwa imetumiwa kugundua ushahidi kuhusu majaribio ya kinyuklia ya Korea Kaskazini.
China imekuwa ikituhumu vitendo vya Marekani karibu na maji hayo yenye utajiri mkubwa yaliopo katika pwani yake ,hatua ambayo imesababisha wasiwasi kati ya mataifa hayo mawili.
- China yarejesha chombo cha Marekani
- China: Marekani itatue mgogoro wake na Korea Kaskazini
- China na Marekani waitisha suluhisho la amani Korea kaskazini
''Uzuizi huo haukufanywa kwa njia ya ''utaalamu'' kutokana na hali ya rubani wa ndege hiyo ya China ikiwemo kasi ya ndege zote mbili'', aliongezea akisema uchungzi wa kijeshi unaendelea.
Mnamo mwezi Februari , ndege moja ya Marekani ilianza kile Washington ilielezea kuwa doria yake ya kawaida kusini mwa bahari ya China ikiandamana na idadi fulani ya meli za kijeshi.
Ndege na meli hizo zilielekea katika eneo hilo licha ya onyo kutoka China dhidi ya kutoa changamoto yoyote kwa uhuru wa China katika eneo hilo.
- China yataka Marekani na Korea Kaskazini kuvumiliana
- China yaionya Marekani kuhusu visiwa vinavyozozaniwa
- China yakamata chombo cha Marekani baharini
Mnamo mwezi Mei 2016 ndege mbili za kijeshi za China zilizuia ndege nyengine ya Marekani iliokuwa katika anga ya kusini mwa bahari ya China.
Wakati huo, jeshi la Marekani lilisema kuwa ilikuwa ikipiga doria ya kawaida katika eneo hilo.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment