Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia) pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo Amina Khamis Shaabani (kushoto) wakijadili jambo kabla ya
kuwasili kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa
(IMF), Tao Zhang katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la
Fedha la Kimataifa (IMF) anaeziwakilisha nchi 23 za Afrika, Bw. Maxwell
Mkwezalamba (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustino Mahiga,
muda mfupi kabla ya kuwasili kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere. Katikati ni Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt.
Philip Isdor Mpango (Mb).
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto), akisikiliza jambo kutoka kwa
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF)
anayewakirisha nchi 23 za Afrika, Bw. Maxwell Mkwezalamba (kulia)
katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere muda mfupi kabla
ya kuwasili kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa
(IMF), Tao Zhang.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kushoto) na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang (kulia) wakifurahia jambo
baada ya kusoma habari kuhusu ujio wa Zhang hapa nchini ambapo alikiri
kutoa taarifa na kusudi la ujio wake zilizoandikwa na Gazeti la Daily
News. Ni muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika
la Fedha la Kimataifa (IMF), Tao Zhang (kulia) akiongozana na mwenyeji
wake Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb),
(kushoto) baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (katikati) na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Tao Zhang (kushoto) waklipeana mkono
walipofika katika moja ya Hoteli jijini Dar es salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)
…………………………..
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika
la Fedha la Kimataifa (IMF) Tao Zhang amewasili nchini kwa ziara ya
kikazi na kupokelewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip
Isdor Mpango (Mb), pamoja na Maafisa wengine waandamizi wa Serikali.
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es
Salaam.
Akiwa nchini, Tao Zhang, atafanya
mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli, Ikulu Jijini Dar Es Salaam
Aidha, Zhang atawasilisha mtazamo
wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF)kwa wadau hapa nchini kwa lengo la
kuifanya Tanzania kuwa na maendeleo endelevu, kuimarisha uchumi mkubwa
(Macroeconomy) na kuwa na uchumi shirikishi.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikaini
Wizara ya Fedha na Mipango
SHARE
No comments:
Post a Comment