Maafisa watatu wa
polisi wameuawa na wengine watatukujeruhiwa katika hsambulio Jumatano
alfajiri eneo la Liboi kaskazini mashariki mwa Kenya karibu na mpaka na
Somalia.
Taarifa katika baadhi ya vyombo vya habari Kenya zinasema kuwa maafisa hao walikuwa wanapiga doria katika eneo la Kulan wakati gari lao lilipokanyaga mlipuko huo.
Maafisa wengine watatu wamejeruhiwa katika shambulio hilo na inaarifiwa wamesafirishwa hadi mjini Nairobi kupokea matibabu maalum.
Katika mtandao wa kijamii Twitter - Shirika la msalaba mwekundu limesema: " gari limekanyaga bomu la ardhini na kuwajeruhi watu 8 baina ya Liboi na Kulan, kaunti ya Garissa."Liliendelea kusema kwamba linashughulikia tukio hilo.
Gazeti la Daily Nation linaripoti kuwa maafisa hao walikuwa wanasafiri kwa gari la kituo cha polisi cha Kulan katika barabara ya Liboi - Milan wakati gari hilo lilipokanyaga bomu la kutegwa ardhini.
Inaarifiwa gari hilo liliharibika vibaya.
SHARE
No comments:
Post a Comment