Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe(kulia) akipokea jezi kwa niaba ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya afrika Lyon Bw.Rajuu Kagenzi(kushoto) mara baada ya kikao na uongozi huo leo Jijini Dar es Salaam. |
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akifafanua jambo
wakati wa kikao na uongozi wa Klabu ya michezo ya Afrika Lyon katika
ukumbi wa Idara ya Habari maelezo leo Jijini Dar es Salaam, kulia ni
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Patrick Kipangula
na kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Klabu ya afrika Lyon Bw.Rajuu Kagenzi.
Mtendaji Mkuu wa Klabu ya afrika
Lyon Bw.Rajuu Kagenzi (kushoto) akiongea wakati wa kikao na Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati)
na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Patrick
Kipangula .
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia)akionyeshwa michora ya
ramani za viwanja vya michezo vinavyotarajiwa kujengwa kutoka kwa
Mtendaji Mkuu wa Klabu ya afrika Lyon Bw.Rajuu Kagenzi(kushoto) leo
Jijini dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe(katikati) akiwa katika picha ya
pamoja na uongozi wa uongozi wa Klabu ya michezo ya Afrika Lyon katika
ukumbi wa Idara ya Habari maelezo leo Jijini Dar es Salaam. (Picha na
Lorietha Laurence-WHUSM)
……………………………………………………………………
Na Lorietha Laurence-WHUSM
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ameupongeza uongozi wa Klabu
ya michezo ya Afrika Lyon kwa kutumia mchezo wa mpira wa miguu
kuelimisha jamii kupambana na ujangili wa tembo.
Waziri Mwakyembe ametoa pongezi
hizo leo Jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na uongozi wa klabu
hiyo katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari
MAELEZO.
Katika kikao hicho uongozi wa
timu hiyo ulimueleza Waziri kuwa timu yao imeamua kushiriki vita dhidi
ya vitendo vya mauaji ya tembo kwa kuandika ujumbe maalum katika jezi za
timu hiyo kuelimisha jamii dhidi ya vitendo hivyo.
“ni jambo zuri kuhakikisha jamii
inapata burudani ya mpira wakati huo huo inaelimika kupitia ujumbe
unatolewa na wachezaji katika jezi zao”Dkt Mwakyembe alisema.
Kwa hivyo, aliushukuru uongozi wa timu hiyo kwa juhudi zao hizo na kukieleza kitendo hicho kuwa ni “cha mfano na kujivunia”.
Aliongeza kuwa Serikali
inajivunia na kuthamini mchango wa wananchi wazalendo wanaojitolea
kujenga taifa na kulinda rasilimali zake kama timu ilivyofanya timu
hiyo.
Aidha Waziri Dkt. Mwakyembe
aliongeza kuwa ni jambo jema linalofanywa na klabu hiyo katika
kuhakikisha inakuza na kuendeleza vipaji kwa vijana mbalimbali nchini
jambo ambalo linasaidia kuinua sekta ya michezo.
Pia aliwapongeza kwa kupata fursa
ya kutembelea nchi ya China kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali
yanayohusu michezo na kuwataka kuitumia fursa hiyo ipasavyo kwa
kujifunza kwa bidii ili watakaporejea waweze kufundisha vijana wengine
wa kitanzania.
Naye Mtendaji Mkuu wa Klabu ya
Afrika Lyon Bw. Rajuu Kangezi ameeleza kuwa mkakati wa klabu hiyo ni
kuhakikisha kuwa inajenga viwanja vya michezo vya kisasa kwa matumizi ya
jamii ili kuendeleza michezo nchini hivyo ameomba ushirikiano na
serikali katika kufanikisha mikakati hiyo.
“Tuna mipango mingi ya
kuhakikisha tunakuwa na viwanja vizuri vya michezo na hili haliwezi
kufanikiwa bila kuishirikisha serikali na viongozi wake hivyo tunaomba
ushirikiano wa serikali katika kuhakikisha tunafanikisha jambo hili”
Katika kikao hicho uongozi wa
klabu hiyo ulimkabidhi Waziri Mwakyembe jezi namba tano “5” ya klabu
hiyo kwa ajili ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli.
SHARE
No comments:
Post a Comment