Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amerejea London kupokea matibabu wiki chache baada yake kukaa huko kwa miezi miwili.
Taarifa kutoka kwa ikulu ya rais huyo imesema amehitajika kwenda Uingereza kuchunguzwa na madaktari.Buhari alijitokeza wakati wa swala ya Ijumaa msikitini katika ikulu wiki iliyopita
Hata hivyo, kufikia sasa hakuna taarifa kuhusu ugonjwa anaougua wala muda ambao anatarajiwa kukaa nchini Uingereza.
Mwandishi wa BBC Tomi Oladipo anasema Jumapili ilikuwa siku muhimu kwa Muhammadu Buhari ambapo alikuwa anakutana na wasichana 82 wa Chibok ambao walikuwa wameachiwa huru baada ya kuzuiliwa na wanamgambo wa Boko Haram kwa miaka mitatu.
Badala yake, kutokana na afya yake, tukio hilo la kuwapokea halikufanywa kuwa sherehe kubwa.
Buhari amekuwa haonekani sana hadharani kipindi kirefu cha mwaka huu.
Alikaa wiki saba Uingereza kabla ya kurejea Machi.
Wiki iliyopita, hakuhudhuria mikutano mitatu ya baraza la mawaziri huku wasiwasi ukiongezeka kuhusu hali yake.
Alijitokeza hata hivyo Ijumaa wakati wa swala ya Ijumaa katika msikiti ulio ikulu ya nchi hiyo.
Buhari alipojitokeza katika ikulu Ijumaa
Taarifa kutoka ikulu imesema kiongozi huyo alikuwa amepangiwa kuondoka mapema Jumapili alasiri lakini akachelewa kwa muda kumuwezesha kukutana na wasichana hao wa Chibok.
SHARE
No comments:
Post a Comment