Na. Immaculate Makilika- MAELEZO
Serikali
imetoa asilimia miamoja ya fedha za bajeti ya dawa kwa mwaka 2016/2017
kwa ajili ya manunuzi ya dawa ikiwa ni moja ya mikakati ya kuboresha
sekta ya afya nchini.
Akizungumza
katika mahojiano ya kipindi cha TUNATEKELEZA kinachoratibiwa na Idara
ya Habari – MAELEZO na kurushwa na kituo cha televisheni cha TBC,
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Dawa Laurean Bwanakunu alisema kuwa
serikali inawahakikishia wananchi kuwa katika mwaka wa fedha 2016/2017
imetenga fedha za kutosha ili kuhakikisha kuwa dawa zinapatikana katika
vituo vya kutolea huduma za afya.
“Ikiwa
ni asilimia 81 ya upatikanaji wa dawa pamoja na vifaa tiba katika
maeneo ya mjini na vijijini, ambapo Bohari Kuu ya Dawa inahudumia vituo
5642 nchi kote” alisema Bwanakunu.
Pia,
Bwanakunu alibainisha kuwa hivi sasa kumekuwepo na upatikanaji wa dawa
muhimu 110 kati ya 135 katika vituo mbalimbali vinavyotoa huduma za
huduma za afya.
Katika
kuboresha huduma za usambazaji wa dawa nchini , Bohari Kuu ya Dawa
imefanikiwa kufungua maduka ya dawa 7 katika mikoa ya Dar es salaam,
Arusha, Geita, Mbeya na Lindi, ambapo imeanza kusafirisha dawa kwa
kutumia ndege na treni ili kufikisha dawa kwa wakati katika vituo
mbalimbali vya afya nchini.
Aidha,
Mikoa na Halmashauri zimetakiwa kuwasilisha maombi yao ya dawa kwa
wakati ili kutatua changamoto ya upungufu wa dawa katika vituo vya
kutolea huduma za afya.
SHARE
No comments:
Post a Comment