Javier
Valdez, aliuwawa na watu wenye silaha ambao walimiminia gari lake risasi akiwa
katika mji wa Culiacán jimboni hapa Kaskazini mwa nchi.
Valdez
(pichani) aliuwawa alipokuwa akiliendesha gari lake kwenda ofisini, kuliko na
mtandao wake wa habari alilolianzisha huko Rio Doce. Mfichuzi huyo aliwahi kufanya kazi katika
Shirika la Habari la AFP na gazeti maarufu nchini La Jornada.
Rais
Enrique Pena Nieto, ameamuru uchunguzi ufanywe kuhusiana na kile alichosema
uhalifu wa kutisha.
AFP
nayo inasema kuwa Valdez alikuwa mtendaji kazi wa hali ya juu hususan katika
shughuli za upekuzi dhidi ya walanguzi wa mihadarati, licha ya kufahamu kuwa
alikuwa anahatarisha maisha yake.
Waandishi
wanne wameuwawa nchini, katika kipindi cha miezi miwili iliyopita.
SHARE
No comments:
Post a Comment