Mkenya aliyefanikiwa kubashiri kwa ufasaha matokeo ya mechi 17 mwishoni mwa wiki amejishindia jumla ya Sh221m za Kenya, ambazo ni sawa na dola 2.2m za Marekani.
Mshindi huyo wa Mega Jackpot ya kampuni ya Sportpesa alianza kushiriki mashindano ya bahati nasibu ya kubashiri matokeo mwaka jana baada ya kutambulishwa kwa mchezo huo na nduguye.
Yeye ni mzaliwa wa pili kutoka mwisho katika familia yenye watoto 12.
Amekuwa akiishi katika mtaa wa Eastlands, Nairobi kwa jamaa yake lakini kwa sasa amepelekwa eneo salama kutokana na wasiwasi kwamba huenda watu wakafika kwa wingi kumpongeza au pengine kutaka kufahamu siri yake.
Kijana huyo alikuwa tayari ameanza kusherehekea alipogundua kwamba alikuwa amebashiri vilivyo matokeo ya mechi 14 kati ya 17 zilizokuwa kwenye Mega Jackpot pale alipopigiwa simu na afisa mkuu mtendaji wa Sportpesa Ronald Karauri muda mfupi baada ya saa sita usiku.
SportPesa, kupitia taarifa, wamesema mshindi huyo alikuwa ameweka dau mara mbili kwa Sh200, kila dau ikiwa ya Sh100.
Samuel alifahamu kwamba mema yalimsubiri baada ya mechi ya Ligi Kuu ya Ufaransa Ligue 1 kati ya Dijon FCO na Bordeaux kumalizika sare 0-0 kama alivyokuwa ametabiri.
Hakuweza kujituliza kutazama mechi mbili zilizokuwa zimesalia kati ya Tottenham Hotspur na Arsenal na mchezo wa Serie A kati ya Inter Milan na Napoli.
"Alienda kwenye klabu viungani mwa mji wa Nairobi ambayo yeye na mwenzake hucheza SportPesa na walikuwa wanajadiliana watafanyia nini mamilioni ya pesa ambayo wangepata pale simu kutoka kwa namba ya simu ambayo hawakuwa wameihifadhi ilipopigwa," taarifa ya SpostPesa inaeleza.
Maafisa wa Sportpesa walimtambulisha rasmi kwa wanahabari Jumanne.
Ili kushiriki shindano la Mega Jackpot, mshiriki huhitajika kuweka dau ya Sh100 pekee za Kenya.
Mechi ambazo mshindi alibashiri kwa ufasaha matokeo yake:
- Sunderland v Bournemouth
- Stoke City v West Ham
- West Bromwich v Leicester
- Barnsley v Burton
- Bastia v Rennes
- Guingamp v St Etienne
- Metz v Nancy
- Montpellier v Lille
- Caen v Marseille
- Bologna v Udinese
- Empoli v Sassuolo
- Everton v Chelsea
- Augsburg v Hamburger SV
- Dijon v Bordeaux
- Tottenham Hotspur v Arsenal
- Inter Milan v Napoli
SHARE
No comments:
Post a Comment