Mfanyibiashara
mwenye hisa nyingi katika klabu ya Arsenal Stan Kroenke anasema kuwa
hisa zake haziuzwi na hazijawekwa katika mauzo.
Kampuni hiyo ya Marekani ilitoa taarifa siku ya Jumatatu kufuatia ombi la pauni bilioni moja la kuinunua Arsenal lililowasilishwa na Alisher Usmanov.
Kampuni ya michezo na burudani ya Kroenke iliongezea kwamba itaendelea kuwa mwekezaji mkubwa wa Arsenal.
Taarifa hiyo inajiri siku moja baada ya Arsenal kushindwa kufuzu katika kinyang'anyiro cha kombe la vilabu bingwa Ulaya kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 20.
Kroenke ana hisa za asilimia 67 katika Arsenal.
Usmanov anamiliki asilimia 30 lakini sio miongoni mwa bodi ya klabu hiyo inayofanya uamuzi.
Raia huyo wa Urusi aliyezaliwa Uzbekistan alisema mnamo mwezi Aprili kwamba Kroenke lazima achukue jukumu la msururu mbaya wa matokeo uwanjani.
SHARE
No comments:
Post a Comment