TRA

TRA

Saturday, May 20, 2017

Tamko la Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !



LEGAL AND HUMAN RIGHTS CENTRE
Justice Lugakingira House, Kijitonyama, P. O. Box 75254, Dar Es Salaam, TANZANIA
Telephone: 2773048, 2773038, Fax: 2773037, E-mail:  lhrc@humanrights.or.tz

TAMKO LA MKUTANO WA 16 WA WANACHAMA
20/05/2017

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kupitia Mkutano Mkuu wa 16 wa Wanachama uliofanyika jijini Dar es Salaam, Jumamosi Mei 20, 2017 kwa lengo la kujadili mwenendo wa kazi za shirika na hali ya haki za binadamu nchini Tanzania kwa ujumla; tumeazimia mambo kadhaa.
Maazimio haya yametolewa na wanachama kufuatia hoja zilizoibuliwa baada ya mjadala wa hali ya Uhuru wa Kujieleza na Uhuru wa Kukusanyika nchini ambayo ndio ilikua dhima kuu ya warsha hiyo.
Hali ya uhuru wa kujieleza na kukusanyika mbali na wadau mbalimbali kupaza sauti, imeendelea kuwa mbaya nchini Tanzania. Vitendo vya vyama vya siasa na wananchi kuzuiwa bila sababu za Msingi vimeendelea kushamiri huku uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa mtu mmoja mmoja kueleza hisia zake ukiendelea kuwa shakani. Wanachama wameazimia yafuatayo:
  1. Kutumia  vyombo vya kikanda na kimataifa ikiwemo Umoja wa Afrika (AU), Umoja wa Mataifa (UN) pamoja na mahakama za kikanda na kimataifa ili kutolea ufafanuzi na kusaidia kwa nafasi yao utatuzi wa hali ya uvunjifu wa haki za binadamu na ukiukwaji wa demokrasia inayozidi kukithiri nchini.
  2. Kuongeza nguvu katika kufungua kesi mkakati ili kuboresha sheria zinazokinzana na haki za binadamu na hatimaye kupata Katiba bora.
  3. Kuendelea kuyajengea uwezo makundi mbalimbali ikiwemo viongozi wa serikali, wabunge, mahakama, jeshi la polisi, viongozi wa dini pamoja na wananchi juu ya umuhimu wa kuheshimu na kulinda haki za Binadamu katika kufanikisha maendeleo ya nchi.
  4. Kudumisha ushirikiano na mshikamano baina ya asasi za kiraia na wadau mbalimbali wa haki za Binadamu ikiwemo vyombo vya habari katika kuifikia Jamii yenye Haki na Usawa.
Tunaamini kwamba kwa Taifa linalojipambanua kuyaelekea maendeleo endelevu halina sababu ya kukandamiza Haki za Binadamu.

Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wanachama wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu hufanyika mara moja kwa mwaka. Mkutano huu wa 16 ulitawaliwa na dhima inayosema “Hakuna Maendeleo bila Uhuru wa Kujieleza na Uhuru wa Kukusanyika”

Imetolewa Jumamosi, Mei 20, 2017
Bi. Anna Henga

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger