Mashindano
ya kombe la Standard Chartered yaliyokuwa yanafanyika nchini Uingereza
yamemalizika na kombe hilo kutwaliwa na timu ya nchini Singapore.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa
kuwasili timu ya Azania iliyowakilsiha nchi za Afrika ya Mashariki,
Meneja Uhusiano wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Mariam Sezinga
amesema timu ya Azania ilikwenda Uingereza kushindana kwenye mashindano
ya “Standard Chartered-Road to Anfield” iliyokuwa inahusisha wateja wa
benki hiyo. Timu zilizoshiriki kwenye mashindano hayo zilikuwa ni timu
nane kutoka Singapore, Uingereza, India, Nigeria, Botswana, Honk Kong,
Korea na Tanzania.
Meneja
Uhusiano wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Mariam Sezinga (nguo
nyeusi) akiwasili na Wachezaji wa Timu ya Azania katika Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam wakitokea
nchini Uingereza kwenye mashindano ya kombe la Standard Chartered-Road
to Anfield 2017.
Katika
michuano hiyo timu ya Azania iliweza kutinga nusu fainali ambapo
ilicheza na Uingereza na kutolewa kwa mikwaju ya penati. Timu ya
Singapore iliibuka mabingwa wa kombe Standard Chartered –Road to Anfield
kwa mwaka 2017. Mariam alisema timu hiyo imefanya vizuri kwenye
mashindano hayo japo hawakufanikiwa kutwaa kombe hilo mara baada ya
kutolewa kwenye michuano hiyo. Alisisitiza wao kama Benki ya Standard
Chartered Tanzania hawajakata tamaa na hii ilikuwa ni fursa nzuri kwa
vijana kuonesha vipaji vyao ili kufikia malengo waliyojiwekea.
Na
pia ameipongeza timu ya Azania kuiwakilisha vyema Tanzania kwa kuwa ni
mara ya kwanza kuingia kwenye mashindano hayo na pia wamejitahidi
kupigana mpaka kufikia kuingia nusu fainali ya mashindano hayo. Nahodha
wa timu ya Azania, Khalid Sultan Said ameishukuru benki ya Standard
Chartered Tanzania kwa kuona umuhimu wa michezo hapa nchini na wameweza
kujifunza mengi kwenye michuano hiyo iliyokuwa ikiendeshwa nchini
Uingereza ambapo timu yao ilitolewa kwenye nusu fainali. Lakini wao
wanaamini hapa ni mwanzo na watapigana mpaka siku kombe liweze kutua
hapa nchini.
Wachezaji
wa timu ya Azania wakiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Mwalimu Julius Nyerere wakitokea nchini Uingereza.
Meneja
Uhusiano wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Mariam Sezinga (wa
tatu kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wachezaji wa Timu ya
Azania mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam wakitokea nchini Uingereza
kwenye mashindano ya kombe la Standard Chartered-Road to Anfield 2017.
Wachezaji
wa Timu ya Azania wakiwasiliana na ndugu jamaa na marafiki mara baada
ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere
wakitokea nchini Uingereza.
SHARE
No comments:
Post a Comment