Mkuu
wa mkoa wa Mwanza John Mongella, akiogea katika kikao hicho cha TRA na
Waandishi wa habari Jijini Mwanza, katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa.
Viongozi wa Tanzania
Chamber of Commerce Mkoa wa Mwanza wakimsikiliza Kamishna wa TRA nchini
wakati wa kikao hicho na waandishi wa habari Mkoani Mwanza.
Kamishna Mkuu wa TRA nchini,Charles Kichere, akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani ( Picha zote na Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Mwanza)
Na Atley Kuni- Afisa habari Mwanza.
Mamlaka ya mapato nchini imetoa
muda hadi kufikia Juni 30, mwaka huu wananchi wote wanaodaiwa kodi ya
majengo kuhakikisha wanailipa kodi hiyo ilikuepuka kufikishwa mahakamani
na kutozwa faini.
Kauli hiyo imetolewa na kamishina
mkuu wa TRA nchini ndugu Charles Kichere, alipokuwa akizungumza katika
mkutano na waandishi wa habari Jijini Mwanza hii leo.
“Mwisho wa kulipa kodi ya
majengo bila adhabu ni tarehe 30 Juni, 2017. Hivyo wenye majengo
yaliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza (Nyamagana), na Manispaa
ya Ilemela wafike ofisi za TRA zilizopo karibu nao kuchukua ankara zao
endapo hawajazipokea kutoka kwa viongozi wa serikali za mitaa yao au
kujisajili na kulipa kupitia benki yoyote ya biashara” alisema Kichere.
Kichere amefafanuakuwa kwa walioko
sehemu ambazo nyumba zimethaminishwa watalipa kiwango cha asilimia ya
thamani ya jengo kama inavyoonesha kwenye ankara zao na walioko maeneo
ambayo hayajapimwa au kuthaminishwa watalipa viwango maalum
vilivyopitishwa na mabaraza ya madiwani na kutangazwa na TRA kwenye
vyombo vya habari.
Kichere amevitaja viwango hivyo
vilivyopitishwa kuwa, ni shilingi za kitanzania (20,000) kwa Jiji la
Mwanza na kumi na tano elfu (15,000) kwa Manispaa ya Ilemela.
TRA pia imepongeza ushirikiano
mkubwa inaoupata kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na safu yake nzima ya
uongozi ikiwemo Serikali za Mitaa husika. “Mhe mkuu wa Mkoa ushirikiano
huo umetuwezesha kutoa makadirio sahihi ya tozo, kutumia viwango
rafiki, kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji, Kutoa elimu kwa jamii,
kushughulikia pingamizi za kodi ya majengo kwa wakati na kuendelea
kuimarisha uthamini wa majengo” amesema Kichere.
Kwa Upande wake Mkuu wa mkoa wa
Mwanza, John Mongella, amesema katika kufikia adhma hiyo ya ukusanyaji
mapato, wakurugenzi wote wa Halmashauri za mkoa huo hawataruhusiwa
kutoka nje ya vituo vyao vya kazi hadi kuisha kwa mwaka wa fedha wa
2016/2017. “Ajenda yetu kuu ni kukusanya Mapato, hivyo Ndugu kamishna
mimi nikuthibitishie tu kuwa kwa sasa, hatuta ruhusu Mkurugenzi atoke
katika kituo chake cha kazi labda kama amepata Msiba” amesema Mongella.
TRA Yatoa siku 39 kodi ya majengo iwe imelipwa Mwanza.
Mamlaka ya mapato nchini imetoa
muda hadi kufikia Juni 30, mwaka huu wananchi wote wanaodaiwa kodi ya
majengo kuhakikisha wanailipa kodi hiyo ilikuepuka kufikishwa
mahakamani, kutozwa faini au vyote viwili.

katika kituo chake cha kazi labda kama amepata Msiba” amesema Mongella

Akijibu maswali ya waandishi wa
habari waliotaka kujua ni kwa namna gani TRA inaweza kufanya ili
kurahisisha mfumo wa malipo kwakutumia mitandao ya simu, amesema wao
kama TRA kila siku hupokea maoni ya wadau ili kuboresha shughuli zao na
kwa hali hiyo wanaona ni wazo jema.
Mamlaka ya mapato Tanzania TRA,
pamoja na majukumu yake imeongezewa jukumu lakukusanya kodi za majengo
ambapo mara baada yakukusanya kodi hizo, zitatolewa taarifa, lakini pia
zitapelekwa kwenye Halmashauri husika kwa ajili ya shughuli za
Maendeleo.
SHARE
No comments:
Post a Comment