Umoja wa Mataifa nchini umeendelea na hekaheka za ufundishaji wa
machampioni wa kusaidia kueneza malengo 17 ya dunia yanayohusu
maendeleo endelevu.
Miongoni mwa mambo yaliyofanywa siku ya pili ya ziara ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez kwa mkoa wa Kilimanjaro na Arusha ni kuendelea kwa mkutano wa vijana unaoakisi Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini Arusha , na kuoongoza kampeni ya elimu ya maendeleo endelevu katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MOCU).
Akiwa MoCU Rodriguez aliwataka vijana kujikita katika kuyaelewa malengo ya dunia na kuyafanyia kazi.
Akifafanua mchango wa vijana katika kufanikisha malengo hayo, Matibu huyo alisema: “Mchango wa vijana ni muhimu katika kufanikisha malengo endelevu kufika mwaka 2030; hivyo ni vyema kila kijana akafahamu na kuwafundisha vijana wenzie malengo hayo muhimu.”
Septemba 2015, wanachama 193 wa Umoja wa Mataifa walikubaliana juu ya malengo mapya ya dunia, malengo ya maendeleo endelevu.
Malengo hayo yanatarajiwa kufanyiwa kazi katika kipindi cha miaka 15 ijayo na kuleta mabadiliko makubwa katika jamii, uchumi na mazingira kwa namna ya kuwa endelevu.
Wakati Umoja wa Mataifa (UN) mwaka jana ukiadhimisha miaka 71 tangu kuanzishwa kwake, Mratibu huyo wa mashirika ya Umoja wa Mataifa aliahidi kuwatumia vijana katika utekelezaji wa malengo yake 17 ya maendeleo kutokana na idadi yao kubwa kubwa zaidi ya asilimia 67 na pia kwa kuwa wao ndio wanaobeba hali ya baadaye ya nchi hii.
Aidha alisema ili kufanikisha hilo, UN pamoja na mashirika mengine itatoa mafunzo ya vitendo kwa vijana zaidi ya 50,000 ifikapo mwaka 2017 ambao wataingizwa katika mpango wa utekelezaji wa malengo hayo.
“UN itaendelea kushirikiana na vijana pia itatoa elimu ya vitendo.Hadi sasa vijana zaidi ya elfu 20,000 wamepewa mafunzo na wanatambua malengo hayo, na kwamba
UN na wadau wengine wanatarajia kufundisha vijana zaidi ya 50, 000 ifikapo mwaka 2017, ili ifikapo 2030 vijana wengi wawe wanajua malengo hayo na namna ya kuyatekeleza,” alisema.
Amesema miongoni mwa mafunzo yatakayotolewa kwa vijana hao ni pamoja na jinsi ya kufanikisha malengo 17 ya maendeleo endelevu na jinsi ya vijana watakavyoweza kujiajiri.
Akiwa Moshi jana, alizungumza na wanachuo na wahadhiri ambapo katika chuo hicho cha MoCU 460 walipatiwa mafunzo na pia walimhoji mambo mbalimbali yanayohusu Umoja wa Mataifa na malengo ya dunia ya maendeleo endelevu.
Kwa mafunzo yaliyofanyika Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira mkoani Arusha Umoja wa Mataifa ulifua vijana 50 ambao ni machampioni.
Aidha idadi ya vijana waliofikiwa na mafunzo hayo kwa kuambukizana wameongezeka na kufikia zaidi ya elfu 20.
Tangu kuzinduliwa kwa kampeni hiyo na mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Alvaro Rodriguez, mwaka jana vijana zaidi wamepata elimu katika maeneo yao kwa kupitia machampioni wa malengo.
Kwa sasa Tanzania imehusisha malengo 17 ya maendeleo endelevu (SDGs) kwenye mpango wa maendeleo wa miaka mitano.

SHARE
No comments:
Post a Comment