Mkuu wa Idara ya Uuguzi Mwanaisha
Juma Fakih akisoma malengo makuu ya warsha hiyo inayowashirikisha
walimu wa Skuli ya afya na sayansi za tiba na viongozi wa wauguzi wa
hospitali za serikali na hospitali binafasi Mbweni.
Kaimu Naibu Mkuu wa Skuli ya Afya
na Sayansi za Tiba Bi. Amina Abdulkadir akimkaribisha Naibu Waziri wa
Afya Harusi Said Suleiman kufungua warsha ya maadili na utafiti kwa
walimu wa skuli hiyo na viongozi wa wauguzi wa Hospitali za Serikali na
Binafsi huko Mbweni, nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Waziri wa Afya Harusi Saidi
Suleiman akisisitiza maadili kwa wafanyakazi wa hospitali na vituo vya
afya wakati akifungua warsha ya siku nne ya maadili na utafiti kwa
walimu wa skuli ya afya na sayansi za tiba na viongozi wa wauguzi katika
skuli hiyo iliopo Mbweni.
Baadhi ya washiriki wa warsha ya
maadili na utafiti wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya (hayupo pichani)
alipokuwa akifungua warsha hiyo inayofanyika Skuli ya afya na Sayansi za
tiba Mbweni.
Kaimu Mkuu wa Skuli ya afya na
Sayansi za Tiba ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar Dkt. Salum Seif akitoa
neno la shukrani baada ya ufunguzi rasmi wa warsha hiyo katika skuli
hiyo iliyopo Mbweni.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya
(wa kati kati) waliokaa katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha ya
maadili na utafiti inayofanyika Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba ya
Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar kilichopo Mbweni, nje kidogo ya Mji wa
Zanzibar.
Picha na Makame Mshenga.
………………………….
Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar
Naibu Waziri wa Afya Bi. Harusi
Said Suleiman ameiagiza Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba ya Chuo Kikuu
cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kufanya tafiti kujua chanzo cha
mmongonyoko wa maadili kwa wafanyakazi wa afya wakati wa kutoa huduma
kwa wananchi.
Alishauri baada ya kupata majibu
ya tafiti hizo kuishauri serikali hatua ya kuchukuliwa ili kuinusuru
hadhi ya taaluma ya afya ambayo inajengeka katika misingi ya ukarimu na
kutoa huduma bila upendeleo.
Naibu Waziri ametoa maagizo hayo
alipokuwa akifungua warsha ya siku nne juu ya Maadili na Utafiti kwa
wakufunzi wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba na viongozi wa wauguzi wa
Hospitali binafsi na Serikali katika skuli hiyo iliopo Mbweni.
Alisema watendaji wa Hospitali na
vituo vya afya na hasa vya Serikali baadhi yao wanakiuka maadili ya kazi
hiyo kwa kuwanyanyasa wagonjwa na kuwatolea lugha mbaya
Alisema tatizo la unyanyasaji
wagonjwa limekuwa kubwa zaidi katika Hospitali kuu ya Mnazimmoja ambayo
ni tegemeo kubwa la wananchi wa Zanaizbar.
Aliongeza kuwa jambo la
kusikitisha ni kuwa wafanyakazi wa hospitali za serikali ambao wamekuwa
wakilaumiwa kwa kukiuka maadili wanapokuwa katika vituo binafsi wanakuwa
ni mfano wa kuigwa kwa tabia njema.
Hata hivyo Bi. Harusi aliwataka
walimu wa skuli ya afya na sayansi za tiba kuwa mfano bora wa maadili na
kuimarisha somo hilo kwa wanafunzi wao ili kurudisha hadhi ya taaluma
ya afya na wananchi waendelee kuwaamini.
Kaimu mkuu wa Skuli ya Afya na
Sayansi za Tiba Dkt. Salum Seif alisema somo la maadli ni moja kati ya
masomo yanayopewa kipaumbele katika skuli hiyo lakini kupata elimu ni
jamabo moja na kuitumia elimu uliyonayo ni jambo jengine.
Alimuhakikishia Naibu Waziri kuwa
watakuwa waangalifu na kuongeza udadisi katika sulala la maadili kwa
wanafunzi wanaomba kujiunga na Skuli hiyo na atakaeonekana hawezi
kukidhi kigenzo watamuacha.
Alisema tatizo kubwa linalochangia
ukosefu wa maadili Zanzibar ni watu kuoneana muhali kutokana na kujuana
sana na kupelekea kuzifumbia macho sheria zilizopo.
SHARE
No comments:
Post a Comment