Wakati Binti Mfalme Sheikha Hamda Alnehayan na binti zake saba wapolisafiri kwenda Brussels, kwa kawaida walikuwa wakikaa katika hoteli ya Conrad. Hiali ilikuwa hivyo pia mwaka wa 2008. Kwa miezi kadhaa familia hiyo ya kifalme ilikodi ghorofa nzima katika hoteli hiyo ya kifahari. Katika muda huo walikuwa na watumishi si chini ya 20, ambao walihakikisha wakubwa zao hawakosi mahitaji yoyote. Walifanya hivyo pasipo kulala, chakula cha kutosha, vibali vya ukaazi wala vya kazi.
Familia Alnehayan ni mmoja ya familia zenye ushawishi mkubwa katika Umoja wa Falme za Kiarabu. Muda mfupi kabla, familia hiyo ilikuwa imenunua klabu ya soka ya Uingereza "Manchester City". Na sasa mabinti hao nane wa Mfalme wanapaswa kujibu mashitaka mbele ya mahakama. Mashitaka yanayowakabili ni biashara haramu ya kuwasafirisha watu na uvinjaji wa haki za kazi.
Wafanyakazi hao walinyanyaswa, walifanya kazi kupita kiasi bila kulipwa
Patricia Le Cocq wa shirika la kutetea haki za binadamu la nchini Ubelgiji linaloitwa Myria katika mchakato wa mashtaka kwa niaba ya wafanyakazi hao wa ndani amesema hawakulipwa ujira wao, walifanyishwa kazi mchana na usiku, walikuwa wakilala sakafuni nje ya chumba cha Binti mfalme na walikuwa mara kwa mara wanatukanwa.
Yote haya yalijulikana pale mmoja wa wafanyakazi hao alipotoroka katika hoteli hiyo na kwenda kupiga ripoti polisi. Kisha ndipo mambo yalipochukua muelekeo huo: Vikosi vya usalama viliweza kuelewa kuhusu hali halisi na kutambua kwamba wafanyakazi hao walikuwa wakiteswa. Uchunguzi wa haraka ulianza. Na mwisho kesi hiyo kuishia mahakamani. Lakini miaka tisa baadaye, familia hiyo ya kifalme inawajibishwa kwa madai yanayowakabili.
Wakati umepita sana kutokana, na utaratibu wa maswala ya kisheria hayo ni kwa mujibu wa muhusika mmoja anyejihusisha na majadiliano. Vyombo vya habari wa Ubelgiji vimeripoti kwamba mwanasheria wa familia hiyo ya kifalme anaukosoa kwa mara kwa mara uchunghuzi wa polisi na kusema kisheria ulikuwa na makosa. Hii ilisababisha safari ya mwaka mzima yenye visa na na mikasa ya kisheria.
Si jambo la kuamini
Mkasa huu haukutambulika hadhrani katika miaka ya hivi karibuni. "Mimi sikuweza kuamini kwamba vyombo vya habari vilitoa taarifa chache sana kuhusu sakata hilo," anasema Nicholas McGeehan wa shirika lakutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch. Mwanasayansi huyo amekuwa akifanya kazi kwa miaka kadhaa katika mataifa ya Ghuba anasema sio malalamiko tu ya kupelekwa wafanyakazi kutoka nchi Ghuba kupelekwa hadi bara la Ulaya bila vibali vya kufanya kazi yna pia wananyanyaswa wakifika huko.
Katika mwezi wa Januari, kesi kama hiyo iligonga vichwa vya habari wakati familia moja ya Dubai ilipokwenda safari na wafanyakazi wao watatu katika mji wa Vienna nchini Austira. Familia hiyo ilifikishwa mbele ya Mahakama ya Haki za Binadamu ya Ulaya kwa makosa ya kuwatesa wafanyakazi wao. Wafanyakazi hao walikimbia na waliwekwa chini ya ulinzi wa shirika haki za bibadamu la nchini Austria mpaka kesi yao iliposikilizwa katika mahakama ya Strasbourg. Lakini Austria na nchi za Ghuba hazina makubaliano ya ushirikiano katika maswala ya kisheria na mpaka sasa watuhumiwa walishaondoka kutoka nchini Ausria.
Kuuondoka umaskini
Wanaharakati wa haki za binadamu wamekemea kwa miaka mingi juu ya "utumwa mamboleo" katika nchi za Ghuba. Kazi hizi hupatikana baada ya wanaume na wanawake kuzipata kupiti kwa mawakala wa ajira katika nchi zao - Bangladesh, India, Sri Lanka au Pakistan. Mawakala hawa huwaahidi kwamba wataondokana na umaskini na wanakwenda katika maisha ya furaha, mishahara ya juu, mazingira mazuri ya kazi na huduma za afya.
Lakini wanapoliwasili Saudi Arabia, Bahrain au Falme za Kiarabu, wengi wao hukumbana na ukweli mgumu. Mara nyingi wao hufanya kazi saa zote na kusubiri kwa muda mrefu mishahara yao. Wakumbwa na mateso ya kupigwa au kutumikishwa kingono. Na kutokana na mfumo unaoitwa ‘'Mpango wa Kafala''ambapo waajiri ndio wanakuwa wadhamini wa wafanyakazi wao kwa hivyo wafanyakazi hao hawezi kutetea haki zao za msingi. Na sheria haiwaruhusu kuacha kazi na kutafuta kazi nyingine kwani hilo huwa ni kosa ambalo mtu anaweza kuadhibiwa na kufukuzwa nchini
Tatizo hili ni la bara Ulaya pia
Ukiukwaji wa haki za binadamu kutoka nje huletwa mpaka Ulaya. Mashekhe wengi husafiri kwenda Ujerumani, Austria au Ubelgiji kwa ajili ya kutafuta matibabu au kufanya kazi. Jinsi wanavyo watendea watumishi wao, pengine inaruhusiwa nyumbani kwao , lakini katika nchi za Ulaya huo huwa ni ukiukaji wa sheria za kitaifa za nchi za Ulaya.
Wakati umefika wa kuonyesha mfano?
Mahakama Ubelgiji sasa ina nafasi ya kutoa mfano katika madai haya . "Kama mahakama itaamua kwamba kuna ushahido wa kutosha juu ya biashara ya binadamu basi watuhumiwa watakabiliwa na adhabu ya kifungo, au angalau fidia kwa waathirika," amesema Patricia Le Cocq, anaelezea wasiwasi wake kwamba labda hata kama watuhumiwa watakuwa na hatia labda adhabu inaweza kuwa dhaifu sana.
Patrick Weegmann mwanasheria maalum wa kimataifa anasema, na kama ni lazima watuhumiwa waje kufungwa hofu inayojitokeza ni kwamba nchi za falme za kiarabu aghalabu hazielekei kuwa zitaweza kuwakabidhi watu waliohukumiwa lakini anasema mwanasheria huyo ana matumaini kuwa kesi hiyo inaweza kuifanya moja ya familia tajiri zaidi duniani kuwajibishwa na kuhusika na biashara ya binadamu na utumwa" Labda sasa itabadili kitu na angalau ukiukwaji wa haki za binadamu katika nchi katika Ghuba utapungua.
CHANZO: DW
SHARE
No comments:
Post a Comment