Habari kutoka
Libya, zinasema kwamba takribani watu 60 wameuawa, katika mapigano
makali kati ya makundi mawili hasimu, Kusini mwa nchi hiyo.
Kundi moja linalojiita Third Force, linasemekana ndilo lililotekeleza shambulio hilo.
Eneo hilo limekuwa likiangaziwa pakubwa kutokana na taharuki inayotanda kati ya wanaounga mkono serikali inayotambuliwa na Umoja wa mataifa iliyoko katika mji mkuu Tripoli, na wapinzani wao.
Mapema mwezi huu, kamanda mkuu wa Libyan National Army, Khalifa Haftar, alikutana na kiongozi mkuu wa serikali iliyopo Tripoli, Bwana Fayez al-Sarraj, ili kujaribu kuzima uhasama unaotokota Kusini mwa nchi hiyo.
Libya iliingia vitani baada ya kuangushwa kwa utawala wa hayati Kanali Muammar Gaddaffi mnamo Oktoba 20 mwaka 2011.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment