K-VIS BLOG/Khalfan Said
KIONGOZI
wa muda mrefu wa Shirikisho la Mpirawa Miguu nchini, (TFF), Alhaji Ahmed
Iddi
Mgoyi, (pichani), ametangaza “kung’atuka kwenye nafasi yake ya Ujumbe wa
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho hilo na kwamba huu ndio muda wake wa
mwisho na
hatagombea tena kwenye uchaguzi ujao.
Mgoyi
ambaye anawakilisha mikoa ya Kigoma na Tabora amekuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya TFF kwa takriban miaka 13 mfululizo
ameweka historia ya kuwa mjumbe mwenye umri mdogo kuliko wote pale alipogombea
kwa mara ya kwanza ujumbe wa kamati ya Utendaji ya TFF.
Alhaji
Mgoyi katika taarifa yake aliyoitoa Juni 13, 2017 amesema, “Pamoja na kuwa bado
nina nguvu uwezo na sifa za kuendelea kugombea lakini pia nimeamini ni wakati
wa kutoa nafasi pana zaidi kwa wengine kugombea na kuwa badala yangu na heshima
kwa fikra nyinginezo. Na ninaondoka nikiwa mjumbe wa muda mrefu zaidi ya wote
kwenye Kamati ya Utendaji inayokamilisha kipindi cha kikatiba na kwa dhati
kabisa naamini kwenye kutoa nafasi kwa wengine.” Amesema Alhaji Mgoyi.
Aidha
Alhaji Mgoyi ambaye pia ameweka rekodi ya kuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya
TFF kwa muda mrefu zaidi kuliko wajumbe wote waliopo sasa, amewaomba radhi wale
wote ambao wangependa au kutarajia kuwa angewania tena nafasi hiyo.
Kama
sehemuya familia ya mpira wa miguu, Alhaji Mgoyi amewashkuru kwa imani yao kwake na bado yupo
nao pamoja.
Hata
hivyo Alhaji Mgoyi ametoa angalizokwa wale wagombea wote wanaoomba kuendelea na
wapya watakuwa wamejiuliza mara za kutosha, wamejipima vya kutosha na
kuzihakiki dhamira zao, wamejiridhisha na wanavyoijua TFF, ukubwa wake na
shughuli zake, wamefuatilia na kutambua vema mahitaji ya mpira wetu,
wametathmini changamoto, madhaifu na makusudi ya kiUongozi na wapo tayari kwa
mabadiliko, wametambua maeneo TFF inayofeli au hayajafanywa vema zaidi na
wanaamini kwenye kuwa sehemu ya ufumbuzi, wamezikataza nafsi zao kufuata
matamanio ya mapenzi ya timu zao, wanafahamu nguzo kuu za mpira wa miguu na
changamoto zinazozikabili na namna ya kuzitatua, utayari wao kujitolea kwa hali
na mali, kuheshimu miiko ya kiuongozi na kuimarisha nidhamu na Uadilifu.
Nimesukumwa
kutoa Ushauri wangu huu kwa kuendelea kuathiriwa na kutoamini sana kwenye
Utekelezaji na Udhibiti wa kimfumo wa
kupatikana kwa Viongozi wa Mpira.. hasa katika ngazi za juu kama hizi
zinazokwenda kugombewa.
SHARE
No comments:
Post a Comment