TRA

TRA

Monday, June 19, 2017

Alichoandika Dk Kigwangalla kuhusu agizo la Mwandoya

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Ninawapongeza sana Halmashauri zote waliotekeleza agizo langu la Mwandoya, Meatu, la kwamba waanzishe huduma za upasuaji kwenye health centers zote zilizopo kwenye Halmashauri zao la sivyo baada ya miezi Sita nitazifutia hadhi health centers zote ambazo hazitokuwa na huduma za upasuaji na kuzipa hadhi ya 'dispensary' ambayo zinastahili(kwa mujibu wa sera ya afya); na kwamba Halmashauri watakaoshindwa kutekeleza agizo hilo viongozi wake kuanzia wakuu wa wilaya, wakurugenzi na waganga wakuu nitawashtaki kwa Mhe. Rais awaondoe nyadhifa zao mara moja. 

Nilitoa agizo hili nikilenga kuimarisha huduma za uzazi na kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi. 

Maboresho yanayokwenda sambamba na agizo hili ni pamoja na uanzishwaji wa huduma za msingi na za lazima za maabara, huduma za Benki ya damu salama na huduma za dharura kwenye ngazi ya kituo cha afya.

  Naibu Waziri wa Afya, Dk Hamis Kigwangalla

Kwamba, badala ya kuwa na Vituo vya afya 'jina' tu, wakati kiuhalisia ni boma la kituo ila huduma ni za ngazi ya 'Zahanati', sasa tuwe na vituo ambavyo ni functional(vinavyofanya kazi halisi ya 'Kituo cha Afya'! Vinginevyo tutashindwa kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi. Sababu ya vifo hivi kutokea ikiwa wazi kabisa na sisi tumeifumbia macho! 

Nilipotoa agizo lile (#AgizoLaMwandoya), nilikuwa serious, sikutania! Kuna Halmashauri wametekeleza, kuna Halmashauri wanasuasua mpaka leo. Bado siku 13 muda wa utekelezaji uishe. 

Nimeipa timu yangu ya ukaguzi miezi mitatu ya kufanya tathmini, kuanzia tarehe 1 July 2017 mpaka September 30, 2017 kisha waniletee ripoti ya Halmashauri zote na mimi nitaandika mapendekezo yangu na kuyawasilisha mbele ya Mhe. Rais kwa hatua za uwajibishaji wa watu wake watakaokuwa wameshindwa kumsaidia kazi. 

Watakaoniita mnoko, sawa, lakini vifo vinavyotokana na uzazi havikubaliki! Mimi nimesema basi - nachukua hatua! Pichani hapa ni kituo cha afya cha mkoani, Halmashauri ya Kibaha Mjini, nikitoa maelekezo ya kurekebisha theatre yao mpya waliyofanyia marekebisho kufuatia #AgizoLaMwandoya .

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger