Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati waliokaa) akishiriki
mazoezi ya Yoga katika maadhimisho ya Mchezo huo hapa nchini
yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
…………………….
Na Shamimu Nyaki – WHUSM.
Wadau wa mchezo wa Yoga nchini
wametakiwa kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi ili wapate kuufahamu na
kushiriki kwa ajili ya kuimarisha afya zao na kuongeza ufanisi katika
kazi zao za kila siku .
Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harisson Mwakyembe wakati wa
maadhimisho ya siku ya Yoga Jijini Dar es Salaam katika uwanja wa
uhuru.
“Nimefarijika kuwa sehemu ya
maadhimisho haya kwani nilikuwa nafikiri Yoga ni mchezo wa misuli tu
lakini leo nimejionea mwenyewe uhalisia wake na jinsi unavyounganisha
akili na mwili kwa pamoja, nawaomba muelimishe wananchi mchezo huu ili
nao waweze kushiriki.” Alisema Mhe. Mwakyembe.
Aidha Mhe. Mwakyembe amewashauri
waandaaji wa mchezo huo kuupeleka Mkoani Dodoma ambapo ndipo makao makuu
ya nchi ili kuwapa fursa viongozi wa Serikali na Wabunge kushiriki kwa
manufaa ya afya na kuongeza utendaji kazi.
Kwa upande wake Balozi wa India
hapa nchini Mhe. Sandeep Arya amesema kuwa Serikali yake itatekeleza
ombi la Mhe. Waziri Mwakyembe la kutoa elimu kwa wananchi kuhusu mchezo
huo ili kuendeleza ushirikiano baina ya nchi hizo.
Mchezo wa Yoga ni mchezo wa
kuchezesha viungo vya mwili lengo lake likiwa ni kuimarisha afya ana
akili na huadhimishwa Juni 18 kila mwaka.
SHARE
No comments:
Post a Comment