TRA

TRA

Friday, June 23, 2017

Alichozungumza Zitto na Balozi wa Indonesia

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
Leo nimekutana na Afisa wa Ubalozi wa Indonesia anayehusika na masuala ya Uchumi. 

Tumejadiliana kuhusu nia ya Serikali ya Indonesia kufanya kazi na Serikali ya Tanzania kwenye kuendeleza zao la Mchikichi.

 Kikao hiki kiliandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania, na Afisa wa Mambo ya nje ndugu Luhangisa alihudhuria mazungumzo yetu. 

Mazungumzo hayo pia yaligusia mahusiano kati ya Mji wa Bojonegoro wa Indonesia na Mji wa Kigoma Ujiji wa Tanzania. 

Meya wa Mji wa Bojonegoro na Meya wa Kigoma Ujiji tayari wana mawasiliano baada ya kukutana kupitia Mpango wa OGP ambao miji miwili hii ni wanachama.
 
Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Mbunge - Kigoma Mjini, ACT Wazalendo
Juni 23, 2017
Dar es salaam

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger