Meneja
Mradi wa kuchakata na kusafirisha Gesi katika Kisiwa cha Songo Songo,
Andrew Hooper (kulia) kutoka Kampuni ya Pan African Energy akitoa
maelezo mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama inayoongozwa na Mkuu wa
Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai (Wapili kushoto) walipotembelea
mitambo ya Gesi Songas iliyopo katika kisiwa hicho juzi.
Ofisa Usalama wa Kampuni ya Pan African Energy inayochakata
na kusafirisha Gesi kutoka Kisiwa cha Songo Songo, Baraka Melchiory (wa
pili kulia) akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher
Ngubiagai (kushoto) kuhusu hali ya usalama na namna ya kujikinga na
majanga pindi itokeapo itilafu katika mradi huo. Mkuu wa Wilaya
aliambatana na Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya katika ziara yake
kutembelea mradi wa Songas juzi.
Mkuu
wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai (Kushoto) akizungumza na
Meneja Mradi wa kuchakata na kusafirisha Gesi Songas katika kisiwa cha
Songo Songo, Andrew Hooper (kulia) kutoka Kampuni ya Pan African Energy.
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa aliambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya
wilaya katika ziara yake juzi.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Zablon Bugingo akizungumza na Meneja
Mradi wa kuchakata na kusafirisha Gesi Songas kutoka Kampuni ya Pan
African Energy, Andrew Hooper wakati wa ziara ya Kamati ya Ulinzi na
Usalama walipotembelea Kisiwa cha Songo Songo kuangalia shughuli
mbalimbali zinazofanywa na kampuni hizo kijijini hapo.
Meneja
Mradi wa kuchakata na kusafirisha Gesi katika Kisiwa cha Songo Songo,
Andrew Hooper (katikati) kutoka Kampuni ya Pan African Energy akitoa
maelezo mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya inayoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai namna mitambo
ya kuchakata Gesi inavyofanya kazi wakati wa ziara yao walipotembelea
chumba maalumu (Control room) katika mitambo ya Gesi Songas iliyopo
katika kisiwa hicho juzi.
Mkuu
wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ndubiagai akizungumza na Viongozi wa
Kijiji cha Songo Songo baada ya kukagua ujenzi ya nyumba ya mwalimu
kijini hapo na kubaini mapungufu kadhaa, mkuu wa wilaya huyo aliambatana
na Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya kutembelea kijijini hapo juzi.
Mkuu
wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ndubiagai akizindua Choo katika Shule
ya Msingi iliyopo katika Kijiji cha Songo Songo kilichojengwa na Taasisi
ya Fanjove, mkuu wa wilaya huyo aliambatana na Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya kutembelea kijijini hapo juzi.
Mkuu
wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ndubiagai akizungumza na wanakijiji cha
Songo Songo baada ya kukagua miradi mbalimbali ya kijiji hicho
iliyojengwa na makampuni yanayo endesha shughuli mbalimbali kijijini
hapo. Mkuu wa wilaya huyo aliambatana na Kamati ya ulinzi na usalama ya
wilaya kutembelea kijijini. (PICHA ZOTE NA VENANCE NESTORY)
SHARE
No comments:
Post a Comment