Mchezaji wa zamani wa klabu ya
Yanga na Taifa Stars Ally Mayay ‘Tembele’ leo Juni 19, 2017 amechukua
fomu ya kugombea Urais wa Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF).
Mayay sambamba na mchezaji
mwingine wa zamani Mtemi Ramadhani walifika TFF kwa ajili ya kuchukua
fomu ambapo Mtemi Ramadhani yeye anawania nafasi ya makamu wa Rais wa
TFF.
Wawili hao walisindikizwa ofisi za TFF na wadau mbalimbali wa soka akiwemo kocha Jamhuri Kiwelu ‘Julio’ pamoja na Jembe Ulaya.
SHARE
No comments:
Post a Comment