Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Augustino
Chacha akizungumza wakati akifungua mafunzo ya awamu ya pili
yanayohusiana na Kanuni za Ukopeshaji katika Kilimo. Mafunzo hayo ya
awamu ya pili yatafanyika kwa siku sita yanaendeshwa kwa pamoja kati ya
TADB, NABAD na MIVARF.
Mkuu wa Idara ya Majanga na
Vihatarishi, Bw. Adam Kamanda (kulia) akizungumza nafasi ya TADB katika
kuwezesha Mabenki na Taasisi za Fedha nchini kuweza kukopesha wakulima.
Meneja Msaidizi wa Mafunzo kutoka
NABAD, Dkt. R.S. Reddy akifundisha namna ya kufanyia uchambuzi miradi ya
kilimo ili kuongeza tija kwenye utoaji wa mikopo kwenye sekta hiyo.
Meneja Msaidizi wa Mafunzo kutoka
NABAD, Bw. M.R. Gopal akifafanua jambo kuhusu nafasi ya NABAD katika
mapinduzi ya kilimo ya India.
Washiriki wa Mafunzo ya Awamu ya
Pili ya Kanuni za Ukopeshaji katika Kilimo wakifuatilia kwa makini
ufunguzi wa mafunzo hayo. Mafunzo hayo yanafanyika katika Hoteli ya
Beach Comber, jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa Mafunzo ya Awamu ya
Pili ya Kanuni za Ukopeshaji katika Kilimo wakiwa katika picha ya pamoja
na wakufunzi na viongozi kutoka TADB.
………………………….
Na mwandishi wetu,
Mabenki yameombwa kuwa tayari
kukopesha mnyonyororo mzima wa sekta ya kilimo na mifugo hili kuunga
mkono juhudi za Serikali za kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza
umaskini nchini.
Hayo yamesemwa na Mwakilishi wa
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania
(TADB), Augustino Chacha wakati akifungua mafunzo ya awamu ya pili
yanayohusiana na Kanuni za Ukopeshaji katika Kilimo yanayoendeshwa kwa
ushirikiano wa pamoja kati ya TADB, Benki ya Taifa ya Kilimo na
Maendeleo Vijijini India (NABAD) na Programu ya Miundombinu ya Masoko,
Uongezaji Thamani Mazao na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF).
Chacha amesema kuwa mabenki na
taasisi za kifedha nchini hazina budi kuwekeza mtaji wa kutosha ili
kuweza kukopesha sekta ya kilimo ambayo ni uti wa mgongo wa Tanzania na
ambayo inaajiri zaidi ya asilimia 75 ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi
nchini na pia kutoa kiasi cha zaidi ya asilimia 65 cha mali ghafi kwa
ajili ya viwanda vya nchi.
Ameongeza kuwa kuanzinshwa kwa
TADB kunalenga kuwezesha mabenki ya biashara kupata fedha zenye masharti
nafuu na endelevu ili ziweze kukopesha sekta ya kilimo ili kuchagiza na
kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha
kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.
“Hakuna haja ya kuogopa kukopesha
sekta ya kilimo kwani ni sekta yenye umuhimu mkubwa kwenye uchumi wa
nchi yetu, TADB kama benki kiongozi ya maendeleo ya kilimo, pamoja na
kuhamasisha mabenki na taasisi nyingine za kifedha kutoa fedha kwenye
mnyororo mzima wa kilimo, imejipanga kusaidia upatikanaji wa fedha zenye
masharti nafuu na endelevu, ili kuinua ushiriki wa wakulima wadogo
katika mfumo wa kifedha,” alisema.
Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya
Majanga na Vihatarishi, Adam Kamanda kwa kutambua umuhimu wa
kuendeleza sekta ya kilimo TADB imejipanga uwa benki ya mfano na ya
kisasa katika kuleta mapinduzi ya kilimo Tanzania kutoka kilimo cha
kujikimu kwenda katika kilimo cha kibiashara na uzalishaji wenye tija
katika kukuza uchumi na kupunguza umaskini.
Bw. Kamanda ameongeza kuwa TADB imejipanga kupunguza changamoto za ukopeshaji zinazoikabili sekta ya kilimo nchini.
SHARE
No comments:
Post a Comment