Mshike mshike wa
michuano ya kombe la mabara umeingia siku ya pili huko nchini Urusi,
ambapo leo kumechezwa michezo miwili ya mashindano hayo
yanayoshirikisha timu nane.
Arturo Vidal na Alexis Sachez wakishangili goli
Mexico walisawazisha goli hilo kupita kwa Javier Hernandez Chicharito na kumfanya mshambuliaji huyu kuwa ndio mfungaji bora wa muda wote wa timu ya taifa akifikisha mabao 48.
Beki Cedric Soares akaongeza bao la pili kwa Ureno katika dakika ya 86 kabla ya Hector Moreno kusawazisha goli hilo kwa upande wa Mexico katika dakika za lala salama.
Katika mchezo wa kundi B wawakilishi wa bara la Afrika Cameroon walichapwa na mabingwa wa Amerika ya kusini, Chile kwa mabao 2-0 mabao ya Chile yalifungwa katika kipindi cha pili na Arturo Vidal na Eduardo Vargas.
CHANZO: BBC
SHARE









No comments:
Post a Comment