
Mkuu wa Wilaya ya Mjini Marina
Joel Thomas akifungua mafunzo ya waandishi wa habari juu ya maradhi ya
kipindupindu yaliyoandaliwa na Idara ya Kinga katika Ukumbi wa RCH
Kidongochekundu Mjini Zanzibar.

Afisa Afya Juma Mohd Juma akitoa
maelezo ya historia ya kipindupindu duniani na hatimae kuingia Zanzibar
katika miaka ya 1976 na kurejea kila baada ya kipindi

Mwandishi wa habari wa Redio
Coconut Tabia Makame akitoa mchango katika mafunzo ya waandishi wa
habari ulioandaliwa na Idara ya Kinga na Elimu ya Afya kuhusu maradhi ya
kipindupindu.

Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Afya
Halima Ali Khamis akieleza malengo ya Wizara ya Afya katika kukabiliana
na maradhi ya kipindupindu ili kuhakikisha yanaondoka Zanzibar.

Daktari dhamana Wilaya ya Mjini
Ramadhani Mikidadi Suleiman akieleza dalili za maradhi ya kipindupindu
Zanzibar na dalili zake katika hatua za awali katika mkutano wa
waandishi wa habari uliofanyika ukumbi wa RCH.

Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo
Zanzibar Hassan Vuai akifunga mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu
maradhi ya kipindupindu katika ukumbi wa RCH Kidongo chekundu.
SHARE
No comments:
Post a Comment