Mahakama nchini
Brazil imemuhukumu gavana wa zamani wa jimbo la Rio de Janeiro, Sergio
Cabral miaka 14 gerezani kwa kuhusika katika rushwa na utakatishaji wa
fedha.
Sergio Cabral alihusika kwa kiasi kikubwa kwenye ujenzi wa miundombinu kwa ajili ya michuano ya Olimpiki
Fedha hizo ni sambamba na zile za makampuni yaliyopata mkataba wa kujenga miundombinu wakati wa michuano ya Olimpiki.
Jaji Sergio Moro ambaye ndiye aliyetoa hukumu hiyo amesema hakuna ushahidi wa kutosha kama mke wa Cabral aitwaye Adriana Ancelmo ambaye pia ni mwanasheria maarufu nchini humo alihusika.
CHANZO: BBC
SHARE









No comments:
Post a Comment