TRA

TRA

Monday, June 12, 2017

GP Sirro: Ni kosa Polisi kudai fedha ya mafuta kwa raia

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !



Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro amewataka makamanda wa polisi mikoa kuhakikisha wanatumia vizuri mafuta ya magari wanayowekewa ili kuepuka malalamiko ya wananchi kwa magari ya polisi kukosa mafuta.

Pia amesema hataki kusikia polisi hawajafika katika tukio kutokana na kisingizio cha kutokuwa na mafuta.

IGP Sirro alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jana mkoani Morogoro na kuongeza kuwa ni kosa kwa mwananchi kudaiwa fedha za mafuta ya gari la polisi.

IGP Sirro yupo katika ziara ya kuangalia hali ya uhalifu katika mikoa akitokea mkoani Dodoma.

Alisema mafuta ya gari yapo katika bajeti ya Jeshi la Polisi kwa kila mkoa hivyo kinachotakiwa ni makamanda wa mikoa kuhakikisha kuwa wanayatumia vizuri.

"Ni jambo la kusikitisha mwananchi kutakiwa kuchangia mafuta ya gari la polisi, hili hatuliruhusu kabisa," alisema Sirro  

Mbali ya suala la mafuta, IGP Sirro aliwatoa hofu wananchi na kusema Serikali inaendelea na uchunguzi wa kina kuhusu mauaji yanayoendelea mkoani Pwani.

"Ni kweli kuna tatizo la mauaji Pwani lakini askari wetu wapo kazini mchana na usiku kutafuta suluhisho la tatizo,"  alisema Sirro.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger