NA K-VIS BLOG
RIPOTI
ya pili ya uchunguzi wa mchanga wa madini, (makinikia), iliyokuwa ikiongozwa na
mchumi, Profesa Nehemiah Osoro, imewaweka matatani vigogo kadhaa wa serikali waliostaafu.
Rais
John Pombe Magufuli tayari ameagiza viongozi hao ukiondoa marehemu Dkt.
Abdallah Kigoda aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, lazima wachunguzwe
na hatua za kisheria zichukuliwe.
Kamati
imesema kulikuwepo na ukiukwaji mkubwa wa sheria ikiwa ni pamoja na uvunjifu wa
sheria uliofanywa na kampuni ya madini ACACIA, na viongozi wa serikali
waliopewa dhamana kusimamia sekta ya madini na hivyo kutoa taarifa zisizo
sahihi na hivyo kulipotezea taifa zaidi ya shilingi Trilioni 300 katika kipindi
chote cha uchimbaji wa madini.
“serikali
ifanye uchunguzi wa dhidi ya waliokuwa mawaziri, manaibu mawaziri wanasheria
wakuu, makamishna wa madini, wanasheria na makampuni ya upimaji wa madini kwa
kuvunja sheria za nchi”. Alisema Profesa Osoro katika mapendekezo ya kamati
Kamati
hiyo ya Profesa Osoro imesema tangu mwaka 1998 hadi Machi 2017, ni makontena zaidi ya 60 na sio 47
kama inavyoonyesha kwenye kumbukumbu za serikali yalisafirishwa nje ya nchi.
Viongozi
wastaafu waliotajwa kwenye mapendekezo ya kamati ni pamoja na Mawaziri wa
zamani wa Nishati na Madini, Mhe. Daniel Yona, Mhe. Nazir Karamagi, Kamishna wa
madini mstaafu Dkt. Dalali Kafumu, Wanasheria wakuu wastaafu, Andrew Chenge na Mwanyika.
Ripoti
pia imependekeza kupitiammsajili wa makampuni serikali ichukue hatua za
kisheria dhidi ya kampuni ya Acacia kwa kuendesha shughuli zake bila usajili.
Mwenyekiti wa Kamati ya Pili ya Wachumi na Wanasheria iliyoundwa na
Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuchunguza Mchanga wa Madini
unaosafirishwa kwenda nje ya nchi, Prof. Nehemia Osoro akiwasilisha
Ripoti ya Kamati yake, mbele Rais Magufuli, Ikulu jijini Dar es salaam
leo Juni 12, 2017.
Mwenyekiti wa Kamati ya Pili ya Wachumi na Wanasheria iliyoundwa na
Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuchunguza Mchanga wa Madini
unaosafirishwa kwenda nje ya nchi, Prof. Nehemia Osoro akiwasilisha
Ripoti ya Kamati yake, mbele Rais Magufuli, Ikulu jijini Dar es salaam
leo Juni 12, 2017
SHARE
No comments:
Post a Comment