Hivi
ndivyo Ufukwe wa Coco (Coo Beach) ulivyofurika watu wa aina mbalimbali
hapo jana jioni, katika kusherehekea sikukuu ya Iddi
pili, mabasi/daladala kutoka kona kadhaa za jiji la Dar zilionekana
zikishusha watu kwa wingi katika ufukwe huo ambao ulisheheni pia vyakula
vya kila aina ikiwemo mihogo,chips mayai na wengine walikutwa na Camera
ya Blogu ya jamii wakiwa wemebeba vyakula vyao na kujibweda kando kando
ya ufukwe,ama kwa hakika ilikuwa burudani kwa wakazi wa jiji la
Dar.Picha na Michuzi Jr.
Kuhakikisha
ulinzi na usalama wa kutosha unakuwepo,Jeshi la Polsi lilipiga kambi
kabisa eneo hilo,kwa idadi ya watu ilikuwa ni kubwa.
Sehemu za kupaki magari zikaonekana hazitoshi kabisa
Foleni
ya kuingia kando kando ya ufukwe nayo ilikuwa kubwa kiasi ambacho
magari mengine yalipita kwa taabu kuendelea na safari zake.
Chopa
ya Jeshi la polisi nayo ilikuwa na kazi ya ziada kama hivi ya kukagua
meneo mbalimbali yaliyokuwa na mkusanyiko mkubwa wa watu,Pichani chini
Chopa ikionekana kwa mbali ilipokuwa ikikatiza maeneo hayo
SHARE
No comments:
Post a Comment