TRA

TRA

Wednesday, June 21, 2017

Jaji afungwa kwa kukaidi agizo la mahakama India

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


 
       Jaji afungwa kwa kukaidi agizo la mahakama. (PRESS TRUST OF INDIA)
 Jaji mmoja nchini India ambaye amekuwa mafichoni tangu ahukumiwe kifungo jela amekamatwa na kufungwa.


Jaji CS Karnan alikuwa jaji wa kwanza wa mahakama kuu nchini India kukabiliwa na kifungo.
Alikamatwa katika jimbo la kusini la India Tamil Nadu siku ya Jumanne usiku.

Alihukumiwa kifungo mjini Kolkata huku ombi lake la kumwachilia kwa dhamana siku ya Jumatano likikataliwa na mahakama ya juu zaidi.

Jaji huyo wa zamani alipatikana na hatia ya kutoa madai dhidi ya majaji wenzake.

Alihukumiwa kwa kukaidi agozi la mahakama na mahakama ya juu zaidi baada ya kutuma barua kwa waziri mkuu Narendra Modi ambapo alimtaka kuwachukulia hatua majaji wenzake.

Alipokonywa nguvu zake kama jaji mnamo Februari. BBC

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger