Meneja Mradi wa kuchakata na kusafirisha Gesi katika Kisiwa cha Songo Songo,
Andrew Hooper (kulia) kutoka Kampuni ya Pan African Energy akitoa maelezo mbele
ya Kamati ya Ulinzi na Usalama inayoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa,
Christopher Ngubiagai (Wapili kushoto) walipotembelea mitambo ya Gesi Songas
iliyopo katika kisiwa hicho juzi.
Ofisa Usalama wa Kampuni ya Pan African Energy inayochakata na kusafirisha Gesi kutoka Kisiwa
cha Songo Songo, Baraka Melchiory (wa pili kulia) akitoa maelezo kwa Mkuu wa
Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai (kushoto) kuhusu hali ya usalama na
namna ya kujikinga na majanga pindi itokeapo itilafu katika mradi huo. Mkuu wa
Wilaya aliambatana na Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya katika ziara yake
kutembelea mradi wa Songas juzi.
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai (Kushoto) akizungumza na
Meneja Mradi wa kuchakata na kusafirisha Gesi Songas katika kisiwa cha Songo
Songo, Andrew Hooper (kulia) kutoka Kampuni ya Pan African Energy. Mkuu wa
Wilaya ya Kilwa aliambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya katika
ziara yake juzi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Zablon Bugingo akizungumza na
Meneja Mradi wa kuchakata na kusafirisha Gesi Songas kutoka Kampuni ya Pan
African Energy, Andrew Hooper wakati wa ziara ya Kamati ya Ulinzi na Usalama
walipotembelea Kisiwa cha Songo Songo kuangalia shughuli mbalimbali
zinazofanywa na kampuni hizo kijijini hapo.
Meneja Mradi wa kuchakata na kusafirisha Gesi katika Kisiwa cha Songo
Songo, Andrew Hooper (katikati) kutoka Kampuni ya Pan African Energy akitoa
maelezo mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya inayoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai
namna mitambo ya kuchakata Gesi
inavyofanya kazi wakati wa ziara yao walipotembelea chumba maalumu (Control
room) katika mitambo ya Gesi Songas iliyopo katika kisiwa hicho juzi.
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ndubiagai akizungumza na Viongozi wa Kijiji
cha Songo Songo baada ya kukagua ujenzi ya nyumba ya mwalimu kijini hapo na
kubaini mapungufu kadhaa, mkuu wa wilaya huyo aliambatana na Kamati ya ulinzi
na usalama ya wilaya kutembelea kijijini hapo juzi.
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ndubiagai akizindua Choo katika Shule
ya Msingi iliyopo katika Kijiji cha Songo Songo kilichojengwa na Taasisi
ya Fanjove, mkuu wa wilaya huyo
aliambatana na Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya kutembelea kijijini hapo
juzi.
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ndubiagai akizungumza na wanakijiji
cha Songo Songo baada ya kukagua miradi mbalimbali ya kijiji hicho iliyojengwa
na makampuni yanayo endesha shughuli mbalimbali kijijini hapo. Mkuu wa wilaya
huyo aliambatana na Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya kutembelea kijijini. (PICHA ZOTE NA VENANCE NESTORY)
SHARE
No comments:
Post a Comment