……………………………………………………………………………
Kampuni
ya simu za mkononi ya Tigo imekabidhi msaada wa chakula na kuandaa
futari kwa ajili ya Watoto wanaishi kwenye kituo cha kulelea watoto cha
Rahaman Ophanage center cha mjini Dodoma .
Msaada
huo ulikabidhiwa jana kwenye kituo hicho na timu ya Wafanyakazi wa
kampuni ya simu ya Tigo Mkoa wa Dodoma ikiongozwa na Meneja wa Tigo
kanda ya kaskazini Aidan Komba .
Akizungumza
wakati wa kukabidhi msaada huo meneja wa Tigo kanda ya kaskazini
inayojumisha mikoa ya Dodoma ,Singida na manyara Aidan Komba alisema
kampuni ya tigo wameamua kutoa msaada huo ikiwa ni sehemu ya
kushirikiana na jamii hasa wenye mazingira magumu.
Komba
alisema msaada huo ni sehemu ya faida ambayo kampuni inarudisha kwenye
jamii kwa kuwaunga mkono katika kununua na kutumia mtandao wao.
Alisema
mwaka huu tigo walichagua kushiriki kuandaa futari na kutoa msaada wa
vyakula kwa Watoto wanaotunzwa katika kituo hicho ili wao
waone kuwa Kampuni inawajali na kushirikiana nao .
Alitaja
aina ya vitu walivyokabidhi hapo jana katika kituo hicho kuwa ni
mchele ,unga wa ngano,unga wa chakula,mafuta ya kupikia na sabuni za
kufulia na kuogea.
Aidha
laisema vifaa hivyo walivyokabidhi thamani yake ni zaidi y ash milioni
1.5 na kuwa vyakula hivyo walivyokabidhi vitasaidia kuendelea kupata
futari kwa siku za kufunga zilizobaki.
Naye
mmoja wa Watoto wanaotunzwa katika kituo cha Rahaman Ophanage Center
cha Chang’ombe mjini Dodoma , Halima Bakari aliwashukuru wafanyakazi wa
kampuni ya tigo kwa kuona umuhimu wa kuwasaidia msaada huo mkubwa.
Kwa
upande wake mwalimu wa kituo hicho Ustadhi Umas Mafita aliishukuru
menejimenti ya kampuni ya Tigo kwa kutoa msaada na kuwapa futari watoto
wa kituo hicho
Alitoa
wito kwa makapuni mengine kuiga mfano wa kampuni ya tigo na
kijitokokeza kukisaidia kituo hicho chenye watoto zaidi ya 100
wanaotunzwa hapo .
Alisema idadi hiyo ya watoto wanaotunzwa pamoja na kupewa mafunzo ya kidini ya kislamu na elimu ya kawaida .
Mafita
aliwaomba tigo kuendelea kuwasaidia kituo hicho kwani kinamahitaji
mengi kama vifaa vya shule,magodoro, vitanda na ujenzi wa mabweni .
SHARE
No comments:
Post a Comment