Serikali
imesema ni marufuku kwa shule ambayo itakuwa haina viwanja vya michezo
kupatiwa kibali cha kufungua shule ikiwa ni utekelezaji wa Sheria ya
Elimu namba 25 ya mwaka 1978.
Akizungumza
wakati wa Ufunguzi wa Masindano ya kwashule za msingi nchini
UMITASHUMTA mkoani Mwanza, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMO) Mh. George Simbachawene, amemuagiza
Kamishna wa Elimu nchini, kutozipatia vibali shule zinazo hitaji
kufunguliwa endapo zitakuwa hazina viwanja vya michezo.
Simbachawene,
amesema kutokana na sheria ya Elimu namba 25 ya mwaka 1978, ambayo
inataka kila shule inapofunguliwa lazima iwe na viwanja visivyo pungua
vitano hivyo nilazima hili lizingatiwe, “nichukue nafasi hii kumuagiza
kamishna wa Elimu kuanzia sasa asisajili shule yeyote ile ambayo itakuwa
haina Viwanja vya michezo, kwani bila kufanya hivyo azma yetu yakuinua
michezo nchini haiwezi kutimia” alisema.
Mbali na kutoa maagizo hayo waziri Simbachawene, ameziagiza pia
halmashauri na wilaya kote nchini kutenga sehemu ya mapato yao ya ndani
kwaajili ya kitengo cha michezo, huku akizihimiza kuweka katika bajeti
ijayo ya serikali fedha kwenye vifungu vinavyo husiana na michezo na
kuonya kuwa endapo Halmashauri itashindwa kufanya hivyo basi yeye kama
waziri mwenye dhamana hatakubali ipite.
Amesema
Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015 sehemu ya (61) inatambua
suala la Michezo lakini pia Sera ya Elimu ya Mwaka 1995, hivyo kama
Serikali lazima waweke kipaumbele katika suala zima la michezo.
Ameongeza
kuwa, Msingi wa Michezo nchini ni michezo ya UMITASHUMTA NA UMISETA
ndio Dira ya timu zetu za Taifa, “Tukiwaandaa vijana wetu vizuri na
kutokana kaulimbiu hii ya masula ya viwanda, hatuna wasiwasi kuwa hawa
ndio viwanda vyenyewe, mchezaji mmoja aliyefikia viwango vya kimataifa
huweza kugharamia hata bajeti ya nchi” alisema Simbachawene.
Katika
hatua nyingine Simbachawene, amewaagiza makatibu Tawala kote nchini,
kusimamia suala la taaluma na michezo, amesema hakuna taaluma bila
Michezo na Hakuna michezo bila Taaluma kwa mantiki hiyo lazima nidhamu
ya hali ya juu iongezwe miongoni mwa vijana na wanamichezo kwa ujumla.
Naye
Mkurugenzi wa Michezo nchini kutoka Wizara ya Habari, Michezo Sanaa na
Wasanii Dkt. Yusuph Singo amesema Tayari Wadau Mbali mbali wa Michezo
wakiongozwa na Chama cha Mpira wa Miguu na Riadha wapo Mkoani Mwanza
kwaajili ya Kuangalia Vipaji kwa ajili ya Timu mbali mbali za Taifa
lakini pia vilabu vyao.
Aidha
amesema kuwa wizara ipo katika Mazungumzo na Timu Manchester City
kupitia wakala wao wa TECHNO kwaajili yakuchukuwa Vijana wapatao kumi
kutoka Tanzania kwaajili yakuwaendeleza kimichezo.
Awali
akimkaribisha Mgeni rasmi, Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella,
aliishukuru serikali kwakuichagua Mwanza kuwa mwenyeji wa mashindano
hayo huku akiomba kwa mwaka ujao mashindano hayo kufanyika tena mkoani
humo, kutokana na madhari mazuri lakini pia ubora wa viwanja na hali ya
ulinzi na usalama inayotamalaki katika mkoa huo, “Mh. Waziri mimi niombe
tu, haya mashindando katika mwaka ujao myalete tena Mwanza sisi tupo
tayari, huo ndio mtazamo wangu lakini pia wenzangu wataniunga mkono”
alisema Mongella.
Mashindano
ya shule za msingi (UMITASHUMTA) ya 2017 ni mashindano ya 22 ambapo
yanashirikisha wanamichezo wapatao 2522 kutoka mikoa 26 ya Tanzania
Bara.
Baadhi
ya Viongozi wa Serikali wakiongozwa na Waziri Ofisi ya
Rais-TAMISEMI George Simbachawene, wakionekana wenye furaha wakati wa
Uzinduzi wa UMITASHUMTA 2017.
Waziri
Ofisi ya Rais-TAMISEMI George Simbachawene, akisalimiana na Kaimu
Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Projestus Rubanzibwa alipofika kufungua
rasmi Mashindano hayo.
Waziri
Ofisi ya Rais-TAMISEMI George Simbachawene akipeana mkono na Katibu
Mkuu Baraza la Michezo la Taifa Mohamed Kiganja wakati wa Uzinduzi wa
UMITASHUMTA 2017.
RUBANZIBWA--
Mh. George Simbachawene, akisalimiana na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa
Mwanza Projestus Rubanzibwa alipofika kufungua rasmi Mashindano hayo.
SHARE
No comments:
Post a Comment