Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MASHINDANO ya Sprite BBall Kings yameendelea tena juzi kwa michezo
mitano kupigwa katika uwanja wa Habours Club Mivinjeni na kufanikisha
kupatikana kwa timu zitakazoungana na zingine za wiki iliyopita.
Hiyo ni raundi ya pili ya mashindano hayo ikiwa ni muendelezo wa
michezo ya mtoano iliyoanza takribani wiki tatu zilizopita ili kumpata
bingwa wa Sprite BBall Kings 2017.
Mchezo wa kwanza uliwakutanisha timu za Mchenga na Ukongana timu
ya Mchenga kuibuka na ushindi wa vikapu 115 dhidi ya 63 za Ukonga.
Mechi ya pili iliwakutanisha Ardhi ambaye alitoka na ushindi wa
vikapu 60 dhidi ya Heroes B aliyepata vikapu 42, Flying D wakaumana na
UDSM na kufanikiwa kushinda kwa vikapu 68 dhidi ya vikapu 45.
Mechi ya nne iliwakutanisha Kigamboni na St Montfort na
ulimalizika kwa vikapu 71 vya Kigamboni dhidi ya 40 vya Montfort huku
mechi ya mwisho ikiwa ni DMI aliyetoka na vikapu 41 dhidi ya 74 vya
Oysterbay na kuhitiMisha michezo ya raundi ya pili ya Sprite Bball
Kings.
Mratibu wa Mashindano hayo ya Sprite BBall Kings Basilisa Biseko
amesema kuwa baada ya kumalizika kwa mechi za wiki hii kutachezeshwa kwa
droo maalumu kwa ajili ha kuzipanga timu zitakazochuana kwenye hatua ya
mtoano ya raundi ya tatu ya Sprite BBall Kings 2017.
"Timu zilizopata alama nyingi katika michezo ya wiki iliyopita na
katika michezo ya ju ndiyo watakaofanikiwa kuingia hatua inayofuata ya
michuano ya Sprite BBall Kings na kutakuwa na droo ya moja kwa moja
itakayorushwa hewani kupanga timu zitakazoumana,"amesema Basilisa.
Michuano hiyo inayodhaminiwa na Sprite kwa kushirikiana na East
Africa Tv na Redio huku mshindi akitarajiwa kuondoka na kitita cha
shiling milion 15.
Timu ya Mchenga (Njano) wakiumama katika hatua ya pili ya michuano
ya Sprite BBalla Kings dhidi ya Ukonga katika mechi iliyopigwa Harbours
Club Mivinjeni na Mchenga kutoka na ushindi wa vikapu 115 dhidi ya 63.
Timu
ya Kigamboni Heroes (wekundu) wakisalimiana na St Montfort kabla ya
mchezo wao wa hatua ya pili ya Sprite BBall Kings uliofanyika katika
uwanja wa Harbours Club Mivinjeni na Kigamboni kuibuka na ushindi wa
vikapu 71 dhidi ya 40
Mohamed
Yusuph mchezaji wa Mchenga akipiga pigo la adhabu kwa timu yake katika
mchezo wa hatua ya pili ya michuano ya Sprite Bball Kings uliomalizika
kwa Mchenga kupata ushindi wa vikapu 115 dhidi ya 63 vya Ukonga.
SHARE
No comments:
Post a Comment