TRA

TRA

Tuesday, June 20, 2017

Kongamano la Kimataifa la Vyombo vya Habari Bonn

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

 

Kongamano linalowaleta pamoja wataalamu wa vyombo vya habari, wanasayansi, wanaharakati na wanasiasa linalofahamika kama Global Media Forum limeanza leo mjini Bonn, Ujerumani.
Kauli mbiu ya kongamano la mwaka huu ni "Utambulisho na Mchanganyiko". 

Katika hotuba yake ya ufunguzi mkurugenzi mkuu wa shirika la utangazaji la Deutsche Welle Peter Limbourg  amesema kongamano hilo la siku tatu linatoa fursa ya  kuangalia nyuma hatua zilizopingwa baada ya  kikao cha kwanza kama hicho miaka kumi iliyopita hapa mjini Bonn. 

Limbourg amesema wakati huo hakukuwepo na changamoto chungu nzima kama zinazoshuhudiwa hivi sasa kwani wakati wa kufanyika kikao hicho  kulikuwepo utulivu maeneo mbalimbali ulimwenguni, hakukuwepo na  mgogoro wa kifedha, umwangikaji damu  hasa mataifa mengi mataifa ya kiarabu, hakukuwepo na idadi kubwa ya wakimbizi wanaohamia  bara la Ulaya, vita vya Ukraine havikuwepo, Donald Trump alikuwa tu na kipindi cha televisheni na ni idadi chache tu ya Waingereza waliokuwa na ndoto ya kujitoa kutoka kwa Umoja wa Ulaya, Brexit.

Limboung amesema nyakati hizi kuna misukosuko zaidi  ambayo inaathiri utendakazi wa waandishi wa habari  na hasa vyombo vya kimataifa vya utangazaji. 

"Kuna uwiano wa moja kwa moja kati ya kiwango cha ukandamizaji wa kitaifa na matumizi ya vyombo vya kimataifa vya utangazaji," mkuu wa DW aliuambia mkutano huo. Watangazaji  wanaonekana kuwa wa kuaminika ndio wanaonufaika.
Brigitte Zypries (Federal Minister for Economic Affairs and Energy, Germany) (DW/P. Böll) Waziri wa uchumi wa Ujerumani Brigitte Zypries akizungumza katika kongamano 

Kuenea kwa taarifa za kupotosha
"Mwaka huu washiriki wa kikao hicho wanaangazia mfumo wa dijitali katika sehemu za kazi," Mkurugenzi wa kongamano hilo la Global Media Forum Patrick Leush alisema. 

Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa uandishi habari unakabiliwa na changamoto kubwa ambapo kila mtu anaweza kutoa habari na kupokea, na hali hiyo inafanya kuwa vigumu kwa vyombo vya habari kuaminika. 

Uaminifu wa vyombo vya habari ni suala lililopewa kipaumbele na washiriki katika kongomano hili na litaendelea kujitokeza kadri mjadala unavyoendelea kutokana na kuenea taarifa za upotoshaji.

Kongamano hilo linahudhuriwa na karibu washiriki elfu 2 kutoka mataifa 130. Kando na waandishi wa habari kutoka Afrika washiriki wengine ni pamoja na wanasisa kutoka hapa Ujerumani, shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa, UNESCO, shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu, Amnesty International, miongoni mwa mashirika mengine.

Tuzo ya uhuru wa kujieleza - Freedom of speech award - mwaka huu inaenda kwa washirika wa vyombo vya habari wa ikulu ya Marekani. Mkurugenzi mkuu wa Deutsche Welle Peter Limbourg amesema uhuru wa kujieleza unapaswa kulindwa ulimwenguni kote kwa sababu ni nguzo muhimu ya demokrasia.

CHANZO: DW

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger