Korea kaskazini imerusha makombora kadha ya kushambulia meli mashariki mwa pwani kwa mujibu wa Korea Kusini.
Makombora hayo yaliruka umbali wa kilomita 200 kabla ya kuanguka baharini.
Marekani inaweka mitambo ya kujikinga nchini Korea Kusini
Majaribio ya makombora ya Korea Kaskazini mwaka huu yamekiuka vikwazo vya Umoja wa Mataifa.
Wataalamu wana hofu kuwa majaribio hayo na hatua za Korea kutundika silaha za nuklia katika vichwa vya makombora.
Msemaji wa Jeshi la Korea Kusini amesema kuw majiribio ya hivi punde yalionyesha kuwa Korea Kaskazini ilitaka kuonyesha kuwa ina uwezo wa kulenga meli kubwa baada ya mazoezi ya hivi majuzi kati ya Marekani na vikosi vya Korea Kusini.
Korea Kaskazini ikionyesha makombora ya Styx 2012
- Uwezo wa kijeshi wa Korea Kaskazini
- Korea Kaskazini: Tutatumia ''silaha kali'' kujilinda dhidi ya Marekani
Lakini hapo awali Korea ilijaribu bila mafanikio kufanyia majaribio makombora ya kushambulia meli.
SHARE
No comments:
Post a Comment