Jeshi la Burma
limesema kuwa mabaki ya ndege yake iliyotoweka Jumatano katika anga ya
bahari ya Andaman ikiwa na abiria 122 wengi wao wanajeshi na familia zao,
yamepatikana.
Ndege hiyo aina ya Y8, iliyotengezwa nchini China, ilikuwa na wahudumu 14 pamoja na wanajeshi 106 na familia wakiwemo watoto.
Ndege hiyo ilikuwa safarini kutoka Myeik ikielekea Yangon.
Ndege hiyo ilikuwa imefanya safari ya nusu saa, wakati ilipoteza mawasiliano siku ya Jumatano.
Picha ya maktaba ya ndege ya jeshi la angani la Myanmar muundo wa Y-8
Ndege hiyo ilinunuliwa kutoka China mwezi Machi mwaka uliopita na tayari ilikuwa imeruka kwa saa 809.
Mynmar imekumbwa na ajali kadha za ndege miaka ya hivi karibuni. Lakini ajali hii ya sasa ndio mbaya zaidi kuwahi kutokea nchini humo.
Mwezi Februari mwaka 2016 watu watano waliokuwa wakisafiri wakitumia ndege ya jeshi, walifariki wakati ndege yao kuanguka kwenye mji mkuu wa Nay Pyi Taw.
Miezi mitatu baadaye maafisa watatu, waliuwawa wakati helikopta ya jeshi ilipoanguka kati kati mwa Mynmar.
SHARE
No comments:
Post a Comment