TRA

TRA

Tuesday, June 20, 2017

Magufuli: Wezi watanikoma

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Mwandishi Wetu

RAIS John Magufuli ameanza ziara mkoani Pwani leo na kusisitiza kuwa wezi watamkoma.

Alisema wapo baadhi ya matapeli walikuwa wananyonya Watanzania kwenye uwekezaji wa umeme huku akibainisha kuwa anachukia wezi na hakuna atakayepona.

"Nachukia wezi, wezi watakoma tu. Awe anatoka Ulaya, Tanzania mwizi ni mwizi tu lazima wale wa chuya," alisema.



Pia alisema serikali imeziba mianya iliyokuwa inapoteza fedha, ikiwemo bandarini kutokana ukusanyaji wa kodi.

Magufuli alisema waliokuwa wanafuja fedha wameshughuliwa na wengine wapo mahakamani. "Fedha za kodi ndizo tunatumia kwenye elimu bure. Tumeanza kulipa madeni ya walimu na  wakandarasi," alisema.

Alisema wameanza kulipa madeni ikiwemo ya walimu na kusisitiza kuwa wenye madeni halali watalipwa.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger