Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya ubashiri wa michezo ya SportPesa Bw. Pavel
Slavkov (kushoto), katikati ni Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji Bw.
Abbas Tarimba.Viongozi hao wa SportPesa walimtembelea Makamu wa Rais
Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa
Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi wa
SportPesa waliofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo kwa
lengo la kujitambulisha.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya
pamoja na Viongozi wa SportPesa Tanzania. (Picha na Ofisi ya Makamu wa
Rais)
………………………………………………………………………
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amekubali ombi la kuwa
mgeni rasmi katika mchezo kirafiki kati ya Timu ya Everton ya nchini
Uingereza na timu ya Gor Mahia ya Kenya ambayo ilitwaa kombe la michuano
ya Sportpesa iliyofayika hapa nchini hivi karibuni.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu
Hassan amekubali ombi hilo baada ya Kukutana na kufanya mazungumzo na
Watendaji wa Kampuni inayojishughulisha na ubashiri wa michezo ya Sports
Betting nchini ambao waliongozwa na Mkurugenzi wa Utawala na
Utekelezaji Tarimba Abbas Ikulu- Dar es Salaam.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu
Hassan amepongeza mipango na mikakati mizuri ya kampuni hiyo ya kutaka
kukuza vipaji vya wanamichezo hasa kwa mpira wa miguu kwa Tanzania Bara
na Zanzibar na kusema kama malengo hayo yatafikiwa Tanzania itakuwa bora
katika mchezo wa mpira wa katika bara la Afrika na Dunia kwa ujumla.
Makamu wa Rais pia
amewahakikishia watendaji wa kampuni hiyo kuwa milango ya ofisi yake ipo
wazi na pindi wakiwama katika jambo lolote wawasiliane na ofisi yake
ili tatizo linalowakabili liweze kutafutiwa ufumbuzi ili lisikwamishe
shughuli za kampuni hiyo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa
Utawala na Utekelezaji wa Kampuni ya Sports Betting nchini Tarimba Abbas
amemweleza Makamu wa Rais kuwa kampuni hiyo ina malengo makubwa ya
kufanya biashara hapa nchini kwa kuzingatia sheria na kanuni za nchini.
Mkurugenzi huyo Tarimba Abbas
amesema katika mipango yao wanataka katika kipindi cha miaka Mitatu
ijayo kampuni yao iwe ni moja ya kampuni bora nchini katika ulipaji wa
kodi kwa Serikali kama wanavyofanya kwa sasa katika Serikali ya Kenya.
Amesema mipango na mikakati
waliyonayo kwa sasa ni kuhakikisha wanainua vipaji vya wanamichezo
nchini kwa sababu Tanzania Bara na Zanzibar kuna vipaji vingi vya
wachezaji wa mpira wa miguu ambavyo haviendelezwi ipasavyo.
Watendaji wa Kampuni hiyo pia
wamemshukuru Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia
Suluhu Hassan kwa kukubali ombi lao na kuwa Mgeni rasmi katika mchezo
wa kirafiki kati ya Timu ya Everton ya nchini Uingereza na timu ya Gor
Mahia ya Kenya mchezo ambao unatarajiwa kufanyika tarehe 13 Julai mwaka
huu katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Utawala na
Utekelezaji wa Kampuni ya Sports Betting nchini Tarimba Abbas amesema
moja ya lengo la kuileta Timu ya Everton nchini ni pamoja na mambo
mengine ni kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii nchini kupitia mchezo
huo ambao unatarajiwa kuangaliwa na maelfu ya watazamaji Duniani kote.
Mkurugenzi huyo pia amemweleza
Makamu wa Rais kuwa tayari wameshawasiliana na mamlaka inayohusika na
masuala ya utalii nchini ili iweze kutumia fursa hiyo kutangaza vivutio
mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini kama hatua ya kuongeza idadi ya
watalii watakaokuja kutembelea vivutio nchini na kuongeza mapato ya
Serikali kupitia sekta hiyo.
SHARE
No comments:
Post a Comment