TRA

TRA

Monday, June 19, 2017

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUTARISHA NA KUTOA VYETI VYA SHUKRANI KWA WADAU WA MAZINGIRA

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Viongozi na Waumini ya Dini ya Kiislam mkoa wa Dar es Salaam wakiwa kwenye sala ya magharibi wakati Iftar maalum iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye makazi yake
Oysterbay jijini Dar es Salaam.
 Raia wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wakisoma Qasida kwenye Iftar maalum iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi cheti cha shukrani Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group Bw. Ruge Mutahaba kwa ushiriki na ufanikishaji wa maadhimisho ya wiki ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa ilifanyika Butiama. Wengine waliopokea vyeti hivyo ni TBC, Lake Gas, TBL, WWF na ZANTAS.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akimkabidhi cheti cha shukrani Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL,Roberto Jarrin  kwa ushiriki na
ufanikishaji wa maadhimisho ya wiki ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa
ilifanyika Butiama.
Wengine waliopokea vyeti hivyo ni TBC, Lake Gas, Clouds Media, WWF na ZANTAS.
Ndugu, Jamaa, Marafiki na Wadau kutoka sekta mbali mbali wakipata futari kwenye
Iftar maalum iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye makazi yake
Oysterbay jijini Dar es Salaam.

                             …………………………………………………………………… 
Makamu wa
Rais wa Jamhuri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amejumuika
na waumini wa dini ya Kiislamu,wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam, viongozi
mbalimbali wa Serikali na wa vyama vya siasa katika halfa ya futari aliyoiandaa
katika makazi yake Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
 
 


Katika Hafla
hiyo ya futari, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia
Suluhu Hassan alishiriki katika utoaji wa vyeti kwa wadau wa mazingira ambao walishiriki
kikamilifu katika maadhimisho ya wiki ya Mazingira Duniani iliyofanyika Kitaifa
tarehe 4-June-2017 – Butiama mkoani
Mara.
 
 


Baadhi ya
taasisi zilizopatiwa vyeti na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ni Shirika
la Utangazaji Tanzania- TBC, Clouds Media, Lake Gas limited, Tbl, Zantas Air na
WWF.
 
 

Akizungumza
kwa Niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu
Hassan katika hafla hiyo ya futari, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais
Muungano na Mazingira, January Makamba alimshukuru Makamu wa Rais kwa kuanda
futari hiyo katika mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwani amesema ni jambo
zuri na linalompendeza Mwenyezi Mungu.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger