Naibu Waziri wa Nishati na Madini,
Dkt. Medard Kalemani akifungua Semina ya Kuwajengea Uwezo Wabunge wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini jijini Dodoma hivi
karibuni. Wengine katika Picha ni Viongozi Waandamizi kutoka Wizara ya
Nishati na Madini na Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi Tanzania
(TGDC).
Naibu Waziri wa Nishati na Madini,
Dkt. Medard Kalemani (mstari wa mbele kushoto) akiwa katika semina ya
kuwajengea uwezo Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na
Madini. Kulia mstari wa mbele ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Nishati na Madini na Mbuge wa Ludewa, Deo Ngalawa na wengine katika
picha ni Viongozi Waandamizi kutoka Wizara ya Nishati na Madini na
Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi Tanzania (TGDC)
Baadhi ya Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakiwa katika Semina ya siku moja jijini Dodoma.
Baadhi ya Viongozi Waandamizi
kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Kampuni ya Uendelezaji wa
Jotoardhi Tanzania (TGDC) wakiwa katika Semina ya siku moja ya
kuwajengea Uwezo Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na
Madini.
Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya
Uendelezaji wa Jotoardhi Tanzania (TGDC), Mhandisi Kato Kabaka akitoa
mada kwa Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini
(hawapo pichani). Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini,
Dkt. Medard Kalemani.
Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa
Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, Kaimu Katibu Mkuu wa Nishati na
Madini Profesa James Mdoe, Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Uendelezaji
wa Jotoardhi Tanzania (TGDC), Mhandisi Kato Kabaka na Kaimu Kamishna wa
Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga. Wengine katika
picha ni Viongozi Waandamizi kutoka Wizara ya Nishati na Madini na
Kampuni ya TGDC.
………………………….
Na Rhoda James – Dodoma
Imeelezwa kuwa Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC) itazalisha Megawati 200-600 kutokana na Jotoardhi ifikapo 2025.
Kauli hiyo imetolewa jijini Dodoma
na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani katika Semina
ya siku moja ya kuwajengea uwezo Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Nishati na Madini.
Dkt. Kalemani ameielezea Kamati ya
Bunge ya Kudumu ya Nishati na Madini kuwa TGDC ina jukumu la kuendeleza
nishati ya Jotoardhi kwa niaba ya Serikali ya Tanzania ili kukuza
uchumi na kuongeza ajira.
Aliongeza kuwa, Tanzania ina reserve
ya Jotoardhi inayokadiliwa kuzidi Megawati 5000 na inapatikana maeneo
mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na Mbeya, Songwe, Rukwa, Dodoma,
Singida, Shinyanga, Morogoro, Pwani, Mara, Kagera na Arusha.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi
wa Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi Tanzania (TGDC), Mhandisi Kato
Kabaka ameieleza Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madini kuwa, Kampuni ya
TGDC ina majukumu mengi likiwemo jukumu la kuendelea kuhimiza matumizi
mengine ya nishati ya Jotoardhi (direct heat use).
Aliongeza kuwa TGDC itaanza
kuzalisha megawati 30 ifikapo 2018 kutoka Mradi wa Ngozi ambapo utafiti
umefanyika kwa kiasi kikubwa.
Mhandisi Kabaka ameelezea
upatikanaji wa jotoardhi ambao unatokana na mchakato wa kinyukilia ndani
ya tufe la dunia, ambalo ni endelevu na mchakato huu hutokea kwenye
nyufa zilizopo kwenye gamba la dunia.
Aidha, ameeleza kuwa tofauti na
upatikanaji wa nishati ya umeme, jotoardhi inajumuisha vitu vingi ikiwa
ni pamoja na gesi ya Carbon oxide, sulphur na madini mbalimbali ambayo
hutumika viwandani na manyumbani.
“Jotoardhi hutumika katika
ukaushaji mazao ya kilimo, uzalishaji wa mbogamboga, ufugaji wa samaki,
utalii wa kibiashara, mabwawa ya kuogelea na usambazaji wa Joto kwenye
Nyuma,” Alisema Mhadisi Kabaka.
Pia, Mhandisi Kabaka alisema kuwa
uzalishaji wa Jotoardhi ni rafiki kwa mazingira ukilinganisha na vyanzo
vingine vya nishati ya umeme.
Mara baada ya Semina hiyo Makamu
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na Mbuge wa
Ludewa, Deo Ngalawa amesema kuwa anaishukuru Wizara ya Nishati na
Madini kupitia Kampuni ya TGDC kwa kuwajengea uwezo katika nishati ya
Jotoardhi na kufahamu faida za nishati hiyo nchini.
Aliongeza kuwa ipo haja ya Kampuni
ya TGDC kuwa na Sheria ambayo itasaidia katika Uendelezaji wa Jotoardhi
na kuagiza Wizara, sasa kuhakikisha kuwa TGDC hailipia leseni ya
utafiti ili kufanikisha zoezi la upatikanaji wa nishati hiyo.
Jotoardhi inazalishwa katika nchi
zaidi ya 26 duniani na zaidi ya Gigawati 12.6 zilipatika mwaka 2015, na
zaidi ya nchi 90 zina maeneo yenye rasilimali ya jotoardhi.
SHARE
No comments:
Post a Comment